Jumatatu, 29 Septemba 2014

JAMBAZI LAUWAWA MORO, LILIKUTWA NA BUNDUKI AINA YA SMG, RISASI NA IRIZI.

 Kamanda wa polisi mkoani Morogoro  Leonald Paul akionyesha suruari  inayofanana na sare ya jeshi la JWTZ ilikouwa ikitumika katika matukio ya ujambazi na Mwantui Anton Msangai. 

Jambazi huyo alifariki dunia baada ya kupata kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali Septemba 29 mwaka huu majira ya saa 12.45 huko katika  eneo la njia panda ya Kilosa.
  Kwa mujibu wa kamanda huyo jambazi huyo alikuwa anaelekea wilayani kilosa kwaajili ya kufanya matukio  ya uharifu.
inadaiwa Septemba 26 jambazi huyo na wenzake walivamia duka moja wilayani Mvomero na kupora 700,00  na vocha za simu na kupiga risasi juu baada ya wananchi kutaka kuwakimbiza,
Kamanda huyo alisema jambazi huyo ni miongoni mwa majambazi watano waliokamatwa na polisi baada ya kufanya matukio ya uharifu mkoani Dodoma na Morogoro.
Kamanda huyo alisema jambazi huyo alikuwa na tabia ya kutumia makundi tofauti ya watu kufanya nao uharifu katika maeneo mbalimbali kisha kutoweka na kuelekea sehemu nyingine.


Kamanda huyo akionyesha bunduki aina ya SMG aliokamatwa nayo Jambazi huyo ikiwa na magazine 2 pamoja na risasi za SMG 47.

 Pia jambazi huyo alikutwa  na irizi ambayo inasadikiwa alikuwa akitumia katika matukio ya ujambazi kwa imani za kishirikina.
  WAKATI HUO HUO 





MTU  mmoja  Joseph Ngasa anashikiliwa na polisi mkoani hapa ,kwa tuhuma za kumbaka  na kumlawiti mtoto wa miaka 7 na kumsababishia kifo chake.

Kamanda wa polisi mkoani hapa Leonald Paul alisema tukio hilo limetokea Septemba 27 mwaka huu huko eneo la Bilo, tarafa ya Ngohelanga wilayani Ulanga.

Alisema  mtuhumiwa huyo alikwenda katika nyumba hiyo kutembea  na kwamba siku ya tukio alikuwa nje, ambapo mtoto huyo alimuaga mama yake anakwenda chooni kujisaidia.

Alisema kijana huyo aliposikia hivyo alimfuata mtoto huyo chooni na kumfanyia kitendo hicho ambapo mtoto huyo alifariki dunia muda mfupi badae.

Alisema mtuhumiwa huyo anadaiwa alifanya kitendo hicho kwa imani za kishirikina, na kwamba  anashikiliwa na polisi atafikishwa mahakamani mara baara ya uchunguzi kukamilika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...