Jumapili, 28 Septemba 2014

MWILI WA MAREHEMU METHOD MENGI KUWASILI JUMATANO UKITOKEA MAREKANI





Marehemu Method Mengi
Mke wa Marehemu katikati akiwa na majonzi






Vitu vilivyotolewa na Watanzania kwa ajili ya mnada



























































Mwili  wa marehemu  Method Mengi mkazi wa Kilakala manispaa ya Morogoro ambaye alikuwa akiishi na kufanya kazi nchini Marekani unatarajiwa kuwasili hapa nchini Jumatano Septemba  mosi mwaka huu ukitokea nchini Marekani.

Mdogo wa marehemu ambaye pia ni Diwani wa kata ya Kilakala Ribon Mkali ,alisema baada ya mwili huo kuwasili ndugu na jamaa wanaoishi Jijini Dar es Salaam watapata fulsa ya kuaga  mwili huo katika uwanja wa ndege wa Dar kisha kuanza safari kuelekea mjini Morogoro.
Aidha alisema  ratiba ya mazishi itaanza saa 5 asubuhi nyumbani kwao Kilakala kwa  chakula, saa 7 kuaga mwili huo  saa 8itafanyika ibada ya kuombea mwili huo katika  kuu la mtakatifu Patric mjini hapa na badae kuelekea katika makaburi ya Kola hili kwaajili ya kukamilisha mwili taratibu za kuhifadhi mwili huo.

Hata hivyo Riboni alipoulizwa juu ya uvumi uliotawala juu ya Marehemu huyo kuuwawa alisema kwa sasa hawezi kuzungumza chochote hadi ripoti ya uchunguzi juu ya kifo cha marehemu huyo itakapokabidhiwa kwa familia.
Marehemu Method  alizaliwa Julai 4,19 72 mkoani Morogoro
 alifariki Septemba 17 mwaka huu nchini Marekani,
Marehemu ameacha mke na watoto watatu,
Mungu ametoa na Mungu ametwaa kazi yake haina makosa, roho ya marehemu ipate rehemu kwa mungu , apumzike kwa amani, Ameen.

 




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...