Jumatatu, 13 Januari 2014

MANISPAA YA MORO INAKISIA KUKUSANYA ZAIDI YA BILIONI 56 MWAKA WA FEDHA 2014/2015

 Meya wa manispaa ya Morogoro Amiri Nondo wakifurahia jambo na naibu meya lidya Mbiaji  baada ya madiwani wa halmashauri hiyo kupitisha bajeti ya shilingi bilioni 56,477,265,443 katika mwaka wa fedha 2014/2015



 Diwani wa kata ya Mbuyuni Samuel Msuya akitoa hoja katika kiao hicho cha bajeti.
 Robon Mkali diwani wa kata ya Kilakala akitoa hoja katika kikao hicho cha bajeti.

 Mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro Simbeye akisoma taarifa katika kikao hicho.
 Wajumbe wa baraza la madiwani la manispaa ya Morogoro wakifutilia kwa makini taarifa ya bajeti hiyo
 Madiwani wa manispaa ya Morogoro wakiwa katika kikao maalumu cha bejeti ya mwaka wa fedha 2014/2015.
 Baadhi ya wajumbe wa baraza la madiwani katika halmashauri ya manispaa ya Morogoro wakiwa katika kikao maalumu cha bajeti.
 Wajumbe wa baraza la madiwani wakifutilia kwa makini kikao cha bajeti.

 Meya wa manispaa ya Morogoro Amiri Nondo akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho.

Meya wa Manispaa ya Morogoro Amiri Nondo wakati akiingia katika kikao hicho cha bajeti..

 
Halmahsuari ya manispaa ya Morogoro inakisia kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 56,477,265,443 ikiwa ni ongezeko la shilingi bilioni 12, 828,572, 796 kutoka katika vyanzo mbalimbali vya fedha.
Meya wa manispa ya Morogoro Amiri Nondo amesema hayo Januari 13 mwaka huu wakati wa kikao maalumu cha bajeti cha baraza la madiwani la halmashauri ya manispaa hiyo.
 Amevitaja vyanzo hivyo kuwa ni  Halmashauri yenyewe, mapato kutoka serikali kuu pamoja na wahisani mbalimbali sambamba na michango ya wananchi katika miradi ya maendeleo ambayo ni shilingi 63,089,832.
Hata hivyo alisema kuwa ongezeko hilo linatokana na kuboreshwa kwa ukusanyaji wa mapato ya stendi kuu ya mabasi ya Msamvu,ongezeko la viwango vya tozo ya kodi na ushuru mbalimbali kwenye masoko, mabango, vibali vya ujenzi na idadi ya mauzo ya viwanja.
Alisema kuwa katika mapato hayo jumla ya shilingi 1,765, 706, 400 zitatumika kwaajili ya uchangiaji wa miradi ya maendeleo sawa na asilimia 37.75 ya makisio, na shilingi 40,473,600 zitalipwa mishahara kwa watumishi wasiopata ruzuku na matumizi mengineyo ni 22,765,786,000sawa na asilimi 65.30.
Pia alisema kuwa kiasi cha shilingi 105,000,000 zitatumika katika vituo vya afya na zahanati mbalimbali katika manispaa hiyo.
Meya huyo alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2014/2015 halimashauri hiyo itatoa kipaumbele katika mambo makuu saba, ambayo  ni mapato, usafi wa mji, utawala bora, elimu, miundombinu na maji

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...