Immaculate Makilika- Maelezo.
SERIKALI
imesema kwamba Benki ya NMB inatarajia kuanzisha utaratibu wa kutuma
ujumbe wa simu kwa wateja kupitia simu zao (Bank massage) pindi mteja
atakapofanya muamala ili yule mwenye akaunti aweze kukubali au kukataa
au kufahamu kuwa kipindi hicho akaunti yake inatoa au inatumika kutoa
fedha.
Aidha,
Serikali imefafanua kuwa imezitaka benki zote kutumia teknolojia ya
kisasa ya (Euro Mastercard Visa-EMV Compliant) ambayo hutumia mfumo wa
“chip based” na kuachana na mfumo wa kizamani unaotumia “magnetic
stripe”. Ambao kwa sasa umepitwa na wakati na ni rahisi kwa wahalifu
kuuchezea na kuiba fedha za wateja.
Hayo
yamesemwa leo Bungeni mjini Dodoma wakati Naibu Waziri wa Fedha, Saada
Mkuya alipokuwa akijibu swali la Kidawa Hamid Saleh(Viti Maalum – CCM)
alipouliza je,Serikali ina mkakati gani wa kupambana na matatizo ya
wizi wa Mabenki kwa njia ya mtandao.
Alisema
kupitia Benki Kuu ya Tanzania imekuwa ikitekeleza mikakati mbalimbali
katika juhudi za kupambana na tatizo la wizi kwa njia ya mtandao.
Aidha
Naibu waziri alisema hatua zingine za kukabiliana na tatizo hili la
mabenki ni kuweka mfumo wa “Anti- Skimming Devices ambapo mfumo huu
unazuia mwizi kugundua namba ya siri ya mteja(PIN), na kwa upande wa
Benki ya NMB imeamua kusimamisha utaratibu wa “swapping” uliokuwa
unatekelezwa na kampuni ya simu ya Airtel.
Katika
swali la nyongeza Kidawa aliuliza pia kama Serikali imewapa adhabu
yeyote wafanyakazi wa NMB na Airtel waliobainika kuhusika na upotevu wa
fedha za wateja na je kama Benki ya NMB itarejesha fedha hizo kwa
wateja?
Mkuya
alijibu maswali hayo kwa kusema kuwa bado hajajua namna gani NMB na
Airtel imewaadhibu wafanyakazi wak, isipokuwa kuhusu kurejesha fedha kwa
wateja ndio NMB inafanya hivyo.
Aidha
Naibu waziri huyo aliendelea kwa kusema Serikali inakamilisha sheria
ya wizi kwa njia ya mtandao (Cyber Crime Act) ambayo itasaidia
kupunguza tatizo hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni