Jumapili, 10 Agosti 2014

VIJANA 30 WA AFRIKA KUSINI WAFURAHIA UHURU WA TZ

Vijana 30  wa vyuo mbalimbali nchini Afrika Kusini wakiwa katika eneo la dakawa ilipokuwa kambi ya  ya waliokuwa wapigania uhuru katika eneo la dakawa wilayani Mvomero, ambao walifika nchini kwaajili ya kujifunza historia ya uhuru wao kama njia moja ya kuazimisha miaka 20 ya uhuru wa Kidemokrasia.
 Timu ya waandishi wa habari kutoka Afrika Kusini waliokuwa katika ziara hiyo.
 mmoja wa vijana hao akiwa katika moja ya darasa katika shule ya sekondari ya Dakawa.
 Mratibu wa Ziara hiyo Bwana Magesa akiongoza safari ya vijana hao kutoka katika eneo la Magadu ambako nako kuna historia ya wapigania uhuru hao.
 Vijana hao wakiwa katika kujadili baada ya kutembelea eneo la Magadu manispaa ya Morogoro.
 Vijana 30  wa vyuo mbalimbali nchini Afrika Kusini wakiwa katika makaburi ya waliokuwa wapigania uhuru katika eneo la dakawa wilayani Mvomero, ambao walifika nchini kwaajili ya kujifunza historia ya uhuru wao kama njia moja ya kuazimisha miaka 20 ya uhuru wa Kidemokrasia.
Waandishi wa habari wakiwa katika eneo la Magadu mjini hapa.
Moja ya mambo ambayo vijana hao wamefurahishwa nayo ni pamoja na uhuru wa nchi ya Tanzania,
Vijana hao kwa nyakati tofauti walikuwa wakishikwa na mshangao kuona wananchi wa Tanzania jinsi wanavyoweza kutembea kwa uhuru masaa yote bila ghubudha yeyote.
walidao nchini kwao huwezi kutembea na kitu cha thamani barabarani bila kupata  msukosuko wowote vinginevyo uwe unajulikana sana.
walisema mara nyingi vitu kama simu na laptop huvitumia wakiwa nyumbani na kisha kutembea hivi hivi.
Pia walifurahia elimu inavyotolewa kwa gharama ndogo hapa nchini ukilinganisha na nchini kwao.
Walishangazwa na watanzania waliozaliwa na raia wa nchi yao kutaka serikali yao kuwasaidia uraia wa nchi hiyo sambamba na elimu jambo ambalo haliwezekani.
walidai hakuna elimu inayotolewa bure na kwamba kila raia wa nchini kwao ni lazima afanye jitiada za kutafura riziki na kwamba sio wanapata bure kama ambavyo watu wengine wanadhania.
Pia walisema suala la kuwepo kwa watoto hao halihusu serikali yao na kwamba hayo yalikuwa ni makubaliano na watu na watu na sio ya nchi,
walisema kwa kipindi baada ya kupatikana kwa uhuru watoto hao walikuwa na maamuzi ya kuchagua kwenda na wazazi wao au kubakia Tanzania.
walisema kwa sasa kutaka nchi hiyo kuwapa uraia ni sawa na kutafuta marumbano na nchi ya TZ ambayo watoto hao ndio raia wake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...