Jumatatu, 4 Agosti 2014

WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA ATAKA JKT KUTOA MAFUNZO KWA VIJANA WAJASILIAMALI


 Naibu waziri wa viwanda na bishara Janeth Mbene akiongea na bwana shamba wa jeshi la kujenga Taifa JKT Philipho Mtui ,  alipotembelea banda hilo katika maonyesha ya wakulima Nanenane mkoani Morogoro.
 Naibu waziri huyo akiwa katika jokofu wa kuhifadhi mboga mboga lililotengenezwa kiasili katika banda hilo la JKT.
 Naibu waziri huyo akiwa katika banda la kuuzia mboga katika banda hilo.
Naibu waziri  huyo akiagana na viongozi wa JKT.
Naibu waziri huyo alishauri JKT kuangalia uwezekano wa  kutumia makambi ya vijana na kuwafundisha masuala ya ujasiliamali ili waweze kujiajiri wenyewe kupitia ujuzi walionao wa kilimo na mifugo.
alisema hayo juzi wakati alipotembelea  banda hilo na kujionesha shughuli mbalimbali zinazofanywa na JKT.
Alisema JKT wanauwezo mkubwa wa kutoa mafunzo kwa vijana hao na kwamba itasaidia vijana hao kuweza kupata ajira na kuepuka kutegemea ajira za serikalini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...