Ijumaa, 2 Mei 2014

WAANDISHI WANAOPATWA NA MAJANGA KUPIGWA TAFU NA MFUKO WA MWANGOSI



Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakiwa katika mkutano wa siku ya uhuru wa vyombo vya habari kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika Jijini Arusha katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC ambapo Mei 3 ndio kilelel cha maadhimisho hayo .
 Wajumbe hao wakifutilia kwa makini mkutano huo wa aina yake .
 Wakongwe katika tasnia ya habari nao walipata fulsa ya kuhudhuria mkutano huo kama wanavyoonekana katika picha.
 Miongoni mwa wajumbe waliohudhuria mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Absalam Kibanda naye alikuwa miongoni mwao ambaye mwaka jana alipata tunzo ya mfuko maalumu ulioanzishwa wa kuasaidia waandishi wa habari wanaopatwa wa majanga ujulikanao kama Mwangosi
 Bujaga Kadago alieyavaa kikoti cha bluu ni miongoni mwa wanataaluma wakonge nchini ambao huwezi kuzungumzia historia ya habari nchini bila kuwagusa
Taasisi mbailmbali zilipata fulsa ya kushirikia mkutano huo  kama wanavyoonekana katika picha,
Habari zaidi soma hapa chini,
Mkurugenzi wa muungano wa clabu za waandishi wa habari nchini Abubakar Karasani amesema mfuko wa kuasaidia waandishi wa habari nchini ujulikanoani kama mfuko wa Mwangosi Media Fund unaandaliwa kuwa kama taasisi maalumu ya kusaidia waandishi wa habari wanaopata majanga hapa nchini,
Alisema mfuko huo utakuwa unalenga kutaoa huduma kwa waandishi wanaopatwa na majanga ya kushitakiwa ambapo watasaidiwa kupatiwa msaada wa kuwezeshwa wakati wa kesi zao.
Pia wale watakaokuwa wakipata matatizo ya kuumizwa wakiwa kazini mfuko huo utawahudumia  kwa kuwapatia matibabu pamoja na huduma zingine katika familia zao.
Kwa wale ambao wanakuwa wapo katika mazingira hatarishi ya kufuatwafuatwa na watu wenye nia mbaya mfuko huo utawawezesha kuwapeleka mahali na kuwahifadhi hadi hapo usalama wao utakapoimarika.
Hata hivyo alisema mfuko huo kila mwaka unatoa tunzo kwa mwandishi bora ambaye amepatwa na majanga  ya kumizwa  na kwamba tunzo hiyo ni tofauti na zingine.
alisema tunzo hizo hutolewa sio kwa kushindwanishwa bali jopo la majaji hukaa na kuangalia kwa makini ni mwandishi gani katika mwaka huo amepatwa na majanga makubwa na hivyo kuweza kumpatia tunzo.
Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Kibanda aliwatupia lawama waharirir wenzake kwa kutokuwa na umoja pale linapotokea tatizo la mwandishi na hivyo kuanza kuwahukumu kuwa ni wanachama wa chama fulani bila kufanya utafiti juu ya jambo kama hilo.
alisema linapotokea janga la mwandishi wahariri hao hukaa pembeni na kuanza kusema hivyo na kuacha kushughulikia matatizo hayo kwa nguvu ya pamoja.
Hata hivyo katika mkutano huo wakati wa majadiliano, suala la maadili lilichukua nafasi kubwa kwa kuwataka waandishi wa habari kujaribu kufanya kazi kwa maadaili ili kuepuka kujidhalilisha kwa kuandika habari zisizo sahihi na hivyo kulazimika kuomba radhi mara kwa mara.
 mada mbalimbali zilitolewa katika mkutano huo ambapo mada iliokuwa na mvuto na kupata wachangiaji wengi ni mada ya Freedom Of Expression in the Cyberspace ( Challenges and opportunities in the Social Media)
ambapo katika mada hiyo mtoa mada Simon Berege kutoka Chuo kikuu cha Iringa aliwataka waandishi wa habari kuwa makini na vitu wanavyoweka katika mitandao ya kijamii kwani mara ngingi vinaweza kuwafanya wakapata mafanikio au kupoteza mwelekeo kutokana na vitu hivyo.
akitolea mfano Berege alisema wapo waandishi wa habari ambao wamekuwa kila wakati wapo katika mtandao na kuweka vitu wanavyofanya jambo ambalo sio zuri sana .
'' Unakuta mtu yuko baa anaweka posti bia ya tatu, ya nne hiyo inashuka hii inaweza kufanya hata wakati unaomba kazi sehemu kuonekana mlevi au uko bz na mtandao  na hivyo kukosa nafasi kwa njia hiyo'' alisema

 Berege alisema kwa utafiti wa mwaka 2012 ulionyesha kuwa Afrika matumizi ya mtandao ni asilimia 7 huku Tanzania kwa sasa utafiti unaonyesha watumiaji ni asilimia 19.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...