Alhamisi, 9 Mei 2013

UTAFITI WA CHANJO YA UKIMWI MBEYA WAENDELEA

dsc_4636
NA MAGRETH KINABO- MAELEZO, DODOMA
WAZIRI wa   Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa  utafiti  wa chanjo ya ugonjwa wa Ukimwi  ijulikananayo kwa jina  la   TAMOVAC -01 katika mkoa wa Mbeya unaoendelea na imeonesha kwamba ni salama  na  ina uwezo wa kusisimua mwili na kuzalisha viini kinga katika dozi ndogo.
 Alisema utafiti huo unaofanywa na Taasisi ya Magonjwa ya Binadamu umewashirikisha watu 60.
  Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma wakati Waziri huyo akiwasilisha  hotuba yake  kuhusu  Makadrio ya Mapato na Matumizi ya fedha kwa mwaka 2013/2014  ya sh. 753,856,475,000 ambapo  aliomba Bunge lijadili kuidhinisha.
  Aliongeza kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2012/2013 wizara yake ilipanua huduma za kinga, matunzo na tiba  kwa ajili ya huduma za VVU/Ukimwi.
 Vituo vya kutolea  huduma ya mantunzo na tiba vimeongezeka kutoka vituo 956 mwaka 2011 hadi kufikia 1,176.  Jumla  watu  1,135,348, wanaoishi na  VVU  wameandikishwa kupata huduma za matunzo,kinga na tiba.
 Hivyo kati ya idadi hiyo wanaopata dawa za kupunguza makali ya VVU ni 663,884 na imeweza kutuoa huduma za wagonjwa wa majumbani kwa wanaoishi na VVU 239,298.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...