Alhamisi, 9 Mei 2013

WABUNGE WATAKA UMOJA KULINDA AMANI, WACHOCHEZI KUDHIBITIWA wabunge

wabunge 
BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   limeazimia kuitaka Serikali kuchukua mara moja dhidi ya viashara  vya aina yoyote ya uvunjifu wa amani unaojitokeza  ilikuwapa wananchi  matumaini ya kujumuika na kubudu kwa uhuru bila kuwa na hofu ya usalama wao. Azimio hilo limepitishwa leo Bungeni kufuatia Mwenyekiti wa  Kamati ya  Bunge ya Ulinzi na Usalama, Anna Abdallah  alipowasilisha Azimio la Bunge la Kulaani Tukio la Kulipuliwa kwa Bomu katika Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olasiti, jijini Arusha , Mei 5,mwaka huu.
“Pamoja na kazi nzuri iliyokwishafanywa na Serikali ya kuwakamata baadhi ya watuhumiwa, Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama kwa kuzingatia majukumu yake ya msingi kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Aprili, mwaka 2013, Kanuni ya 118 ikisomwa  pamoja na nyongeza na Nane, Kifungu cha 6(3),.
  “Inaomba kuleta azimio la kuitka Serikali na vyombo vyote vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa inatumia uwezo wake wote kuendeleza uchunguzi wa kina na kuwatia nguvuni wale wote waliohusika na tukio hili kubwa na la kinyama na kuwafikisha katika vyombo vya sheria haraka iwezakanavyo ili hatua kali zichukuliwe dhidi yao,” alisisitiza.
  Akichangia azimio hilo, Mbunge wa  Jimbo la Kigoma Kaskazini-CHADEMA Kabwe Zitto alisema  tunaweza kuwa na sheria ya kupiga marufuku lugha za uchochezi kwa Watanzania zinazoweza kuligawa Taifa.
“Mikanda inauzwa hadharani inawagawa Watanzania tunaomba kipengele hiki kamati iingize katika azimio  wanasheria watatusaidia,” alisema Zitto.
 Mbunge wa Jimbo  la  Kibakwe – CCM George Simbachawene alisema; “inaweza  kuwa  ni fursa na kauli zetu tunazotoa kama viongozi wa dini au kisiasa kwa wengine tunawapelekea ujumbe inakuwa ni mapambano”, .
  Kwa upande wake   James Mbatia – NCCR Mageuzi aliiomba Serikali isimamie sheria zilizopo.
 “Wanasiasa   tuna mkono wetu mkubwa kwa yeyote ni wajibu wetu sote usitake kupata maradaka kwa kumwaga damu ya Watanzania. Nawaomba Watanzania tuwe kitu kimoja,” alisema Mbatia .
 Naye Mbunge  Jimbo la Vunjo –TPL Agustino Mrema alitaka jamabo linapotokea hatua zichukuliwe mara moja.
 Aliongeza kuwa wahubiri wanaopewa kibali cha kuhubiri  na wanatukana na kutoa lugha za uchochezi, vikundi au madhehebu vichukuliwe hatau, ambapo alitoa siku saba.
 Mbunge wa Viti Maalum – CCM Getrude Rwakatare aliomba viongozi wa dini kuhuri upendo.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Utaratibu ,  Stephen Wassira, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bunda – CCM ,aliwashauri wabunge kuungana pamoja ili kushinda tatizo hilo.
 “ Waliopatikana watatusaidia Serikali , hakuna atakayepona Serikali itachukua hatua.  Tunaendelea na kazi hiyo hadi nchi inakuwa na amani,” alisema Waziri Wassira.
 Mwenyekiti  wa kamati hiyo  alisema suala la kupitia sheria ni la msingi na kamati hiyo italiangalia. Pia aliongeza hata lugha ya uchochezi hata Bungeni hairuhusiwi kwa pande zote.
 “Jambo hili halifai tumeanzisha sisi humu ndani wimbo watu wanaitikia. Lazima  tuilinde nchi kwa udi na uvumba.
 ”Hakuna  kiongozi atakayechaguliwa kwa udini nchi hii lazima achaguliwe na Wakristo na Waislamu,” alisema.
 Spika wa Bunge hilo, Anne Makinda aliwataka  wabunge kuchunga kauli zao.
 Katika hatua nyingine spika huyo aliondoka kwenda Arusha kwa safari ya siku moja na baadhi wa wabunge ili kutoa pole kwa wananchi wa Arusha.max=2013-05-08T21:30:00-07:00#ixzz2SnhibdU7

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...