Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Chistine Ishengoma akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) mkoa wa Iringa kilichofanyika kwenye ukumbi wa Siasa ni kilimo, Manispaa ya Iringa. (HM)
Wajumbe wa kikao cha RCC
MKUU wa mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma ameziagiza Halmashauri mkoa wa Iringa kuhakikisha wanasimamia vema fedha za miradi zinazotolewa na serikali katika maeneo yao. Mkuu huyo wa mkoa ametoa agizo hilo leo katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo wakati akifungua kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC).
Amesema kuwa lengo la serikali kutuma fedha za miradi katika Halmashauri husika ni kuwezesha kusukuma mbele kasi ya miradi ya maendeleo katika Halmashauri. Hivyo alisema haitapendeza kuona fedha za miradi katika Halmashauri zinakosa usimamizi mzuri na kupelekea miradi kukwama kumalizika kwa wakati.
Alitaka viongozi wa Halmashauri kubuni miradi ya kuziwezesha Halmashauri zao kuongeza mapato zaidi.
Alisema bila ya Halmashauri kubuni miradi ya kiuchumi uwezekano wa Halmashauri kujiendesha utakuwa mdogo zaidi.
Alisema watumishi wasiojituma katika kazi mkuu wa mkoa ametoa onyo kwa watumishi hao na kuwa kamwe hata wavumilia. Katika hatua nyingine mkuu huyu wa mkoa ametoa agizo kwa jeshi la polisi mkoa wa Iringa kupitia askari wake wa usalama barabarani kuwakamata na kuyakamata na kuyatoza fani magari yote ya abiria ambayo yatapita katika mkoa wa Iringa bila kuwa na vifaa vya kuhifadhia taka na yale yatakayobainika yakichafua mazingira ovyo. Chanzo: Francis Godwin
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni