WANANCHI wa Kijiji cha Madege kata ya Chakwale wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro Wameiomba Serikali
kuwajenga daraja la Mto Kibedia ili kuwanusuru maisha yao hususani wakati wa
mvua.
Wananchi hao walisema hayo jana wakati wa ziara ya viongozi wa chama cha Mapinduzi
CCM mkoa wa Morogoro waliotembelea katika kijiji hicho kwa lengo la kukagua ilani ya uchaguzi.
Mmoja wa wananchi kutoka kata hiyo ya Chakwale Mwidadi
Ibarahimu alisema kuwa daraja hilo halina kivuko na kwamba wananchi wake huvuka
kwa shida hali inayosababisha kila mwaka vifo kwa wanancho wanaotumia mto huo.
‘’ kutokana na kutokuwa na kivuko katika mto huu, wananchi
wanapoteza maisha, unakuta maji yamejaa ghafla na watu wako ng’ambo ya pili na
kwamba wanapojaribu kuvuka huzolewa na maji’’ alisema.
Hata hivyo wananchi hao wamelalamikia pia barabara ya Iyogwe
inayounganisha na wilaya ya Kilindi mkoani Tanga kujengwa nyembamba
ukilinganisha na ile inayokutana na ya Ngiloli
huko Kilindi.
Walisema kuwa barabara hiyo ni moja ya ahadi ya Rais wakati
wa kampeni za uchaguzi wa mwaka 2010
ambapo aliwaambia imependishwa hadi na kuwa ya Tanroad badala ya Halamshauri kama ilivyokuwa awali.
Kwa upande wake Hasan
Chobo alisema kuwa pamoja na kuwa barabara hiyo ni ya kiwango cha
changalawe lakini ilipaswa ijengwe kwa viwango vinavyosatahili ikiwa ni pamoja
na kuwa na mifereji ya kupitisha maji ya mvua pamoja na upana unaokidhi
mahitaji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni