VIONGOZI wa
chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema katika serikali ya kitongoji cha Mgudeni kijiji cha
Mkangawalo, kata ya Mngeta wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro wamelalamikiwa kuwafanyia
vitendo vya unyanyasaji wananchi wa eneo hilokuwapakia katika pikipiki na kuwafunga pingu mikono katika machuma ya
pikipiki .
Wananchi hao
walisema hayo jana kwenye mkutano wa hadhara
wakati wa ziara ya katibu wa chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Morogoro
Rojas Romuli uliofanyika katika kitongoji hicho cha Mgudeni
Wananchi hao
walisema kuwa viongozi hao wa Chadema ambao wengi ni viongozi wa serikali ya
kijiji hicho kwa kushirikiana na afisa mtendaji aitwaye Rajabu Kipolelo wamekuwa wakiwafanyia wananchi wa eneo hilo
vitendo hivyo pale mwananchi anaposhindwa kulipa faini mbalimbali kijijini
hapo.
Mmoja wa
wananchi ambaye aliwahi kufanyiwa unyanyasaji huo Maduka Mwela alisema kuwa
yeye alitakiwa kulipia kiasi cha shilingi 300,000 kama malipo ya kodi ya ardhi
na kwamba alitoa shilingi 180,000 za awali lakini cha kushangaza siku iliyofuata
alikuta amewekewa alama ya msalaba
mwekundu katika shamba lake kisha kufuatwa na askari mgambo na kumkamata.
Alisema kuwa
mgambo hao walimfunga mkono mmoja nyuma ya pikipiki baada ya kumpakia na kisha kuondoka naye hadi
kwa mtendaji huyo wa kijiji.
‘’
Nilipofika mtendaji huyo alinipokea kwa maneno ''nyinyi ndio mnakaa vikao na chama chenu cha CCM halafu mnapinga kulipa ada ya ardhi'' Tulibishana kwa masaa kadhaa ‘’ Alisema
Alisema kuwa
wananchi wa kijiji hicho baada ya kuona tukio hilo waliandamana hadi katika
ofisi ya mtendaji huyo kushinikiza mwenzao huyo ambaye ni balozi wa CCM aachiwe na ndipo afisa huyo
alipomwachia.
Kwa upande
wake Richard Mwamwanga ambaye ni mjumbe katika serikali hiyo ya kijiji ya mseto
alisema kuwa viongozi hao wamekuwa wakijipangia bei za ada kinyume na utaratibu
kwa lengo la kuwakomoa wananchi.
Alisema kuwa
awali wakati serikali ya kijiji hicho ilipokuwa ikiongozwa na CCM walikuwa
wakilipia ardhi kiasi cha shilingi 20,000 ambapo walipoingia wao madarakani
walipandisha hadi kufikia 40,000 kwa hekari.
Hata hivyo
mjumbe huyo alisema kuwa mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho ambaye
anatokana na chama cha Chadema Stelatoni Njaani amekuwa akiongoza kwa njia ya
udikteta kutokana na kwamba maamuzi anayoamua yeye na wenzake wa Chadema hataki
mtu mwingine atoe hoja ya kuhoji.
Naye Deus
Makaranga, katibu wa baraza la wazee kijijini hapo alisema kuwa viongozi hao kwa
kushirikiana na mtendaji huyo wamekuwa wakitoa risiti feki katika kulipia
mashamba pamoja na michango mbalimbali ya maendeleo.
Alisema kuwa
wamekuwa wakitumia risiti moja kuandika mchango zaidi ya mmoja sambamba na
kutoa risiti kwa watu tofauti zenye namba
zinazofanana.
Kwa upande wake Gidius Alois Mwagombeka
alisema kuwa yeye alikuwa mweyekiti wa kijiji cha Mkangawalo na kwamba viongozi hao
wa Chadema walimfanyia hila kwa kumtuhumu kufanya ubadhilifu wa fedha za
maendeleo katika kitongoji hicho hali
iliofanya mkuu wa wilaya ya Ulanga Francis Miti ambaye alikuwa akikaimu wilaya hiyo baada ya
mkuu wa wilaya hiyo Evarist Ndikilo
kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa kumwondoa madarakani.
Alisema kuwa
hiyo ilikuwa mwaka 2012 na kwamba tume iliundwa katika kitongoji hicho dhidi ya
tuhuma hizo na kubaini kuwa sio za kweli.
Mwisho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni