Jumatatu, 13 Januari 2014

CCM YAMREJESHA MZERU KUGOMBEA UDIWANI TUNGI

 Huyu ndiye  Deogratias Mzeru , mgombea udiwani mteule wa chama cha mapinduzi CCM katika kata ya Tungi manispaa ya Morogoro, ameteuliwa  Januari 13 mwaka huu. baada ya kamati ya siasa ya mkoa wa Morogoro kuketi.

 Safari ya kwenda Tungi ilivyoanza, ilikuwa ni safari ya kwenda kumsindikiza mgombea udiwani mteule wa kata hiyo kuchukua fomu ya serikali ili kuingia katika kinyang'anyiro hicho.

 Hapo wazee wa kata ya Tungi wakimsindikiza kijana wao Mzeru kwenda kuchukua fomu ya kugombea udiwani katika ngazi ya serikali.

 Ni katika ofisi ya afisa mtendaji wa kata ya Tungi, Mzeru akiangalia kwa makini fomu alizopewa kwaajili ya kuomba ridhaa ya kuwa diwani wa kata hiyo.

 Wiii, waaaaa, vijana wangu wote mmeenea, sasa tuanze mchakamchaka, ni maneno ya mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Morogoro Salamu Mkolwe wakati za zoezi la kuchukua fomu kwa mgombea udiwani wa kata ya Tungi.

 Tunashukuru sana afisa mtendaji wetu, acha sasa tukajaze fomu hii, tuterejesha kesho mapemaaaa.

 CCM ahaaaa, CCM inawenyewe, chezea CCM weye, haaaahaaa, ni maneno ya makada mashuhuri manispaa ya Morogoro yaliokuwa yakisikika wakati wa ndremo hiyo katika ofisi ya mtendaji wa kata ya Tungi.

 CCM ninavyoipenda nitakunywa sumu juu yake, makada wa CCM wakiserebuka .

 Siami chama weee, siamii, na mzeru yupo weee, siami, makada wakiimba wakifurahia wakati wa diwani mteule mzeru akichukua fomu ya serikali kuwania udiwani kata ya Tungi.

 Mgombea Udiwani wa kata ya Tungi Mzeru, katibu wa UWT Dotto na katibu wa CCM wilaya Ali Isa  wakiteta jambo na mgombe huyo.

 Tumekuja manispaa kukamilisha taratibu zingine za kiutumishi.

 Mgombea udiwani Mzeru akiwa katika taratibu za kukamilisha mambo fulani ya kiutendaji.

 Mke wangu, umekuja kuniunga mkono mama, asante mwaya, nimeshachukua fomu tayari ngoja nikajaze, si unajua muda wenyewe uliobakia mdogo. 

 Sisi kwa pamoja tunakuunga mkono, tunakutakia kila la kheri. ni wananchi wa kata ya Tungi wakiwa katika picha ya pamoja na mgombea udiwani wao.

 Kila cheleko ina mwenye, wazee wa kata ya Tungi wakimsindikiza kijana wao mara baada ya kuchukua fomu.
 Ni mimi jamani Mzeru wa CCM, naomba ushirikiano wenu, kwa pamoja tutashinda.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...