Jumapili, 9 Februari 2014

MANGULA ATAKA WANAOSALITI CCM WAFUKUZWE UANACHAMA

 Makamo mwenyekiti wa CCM Tanaznia Bara Philip Mangula akiongea katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Tungi.


 Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Rojas Romuli akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo.
 Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Aziz Abood akiongea wakati wamkutano huo

 Meya wa manispaa ya Morogoro Amiri Nondo akiomba kura za Udiwani kata ya Tungi.

 Katibu wa CCM wilaya ya Morogoro mjini Isa Ali akiongea wakati wa mkutano huo
 Wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa na wilaya Morogoro mjini wakati wa kikao cha Halmashauri kuu ya wilaya hiyo
 Wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya ya Morogoro wakifutilia kikao hicho
 Wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya hiyo
 Hao ni kundi la vijana la hamasa la Nyota tatu wakiwa katika burudani katika mkutano wa kampeni za udiwani Tungi
Hawa nao ni kikundi cha burudani cha Mabadiliko wakila kiapo cha CCM.


habari kamili soma hapa chini.
CHAMA cha Mapinduzi CCM kimesema kuwa mtu anayekisaliti chama adhabu yake ni kufukuzwa uanachama  na kwamba chama kinapaswa  kufanya hivyo kwa watu hao ili kujenga heshima.
Makamo Mwenyekiti wa CCM Taifa Tanzania bara Philip Mangula alisema hayo jana wakati wa kikao cha halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Morogoro mjini ambayo pia ilihidhiliwa na wajumbe wa kamati ya siasa na sekretarieti ya mkoa huo.
Alisema kuwa amelazimika kusema hayo baada ya kupokea taarifa kuwa wapo baadhi ya viongozi na wanachama ambao wanasaliti chama kutokana  mtu waliyemtaka katika udiwani kata ya Tungi jila lake halikurudishwa.
Alisema kuwa  hakuna budi kuwashughulikia watu hao ambao wanakiharibu chama kwa manufa ayao binafsi na kuahidi kurejea Morogoro kwaajili ya kuwashughulikia watu hao.
‘’ Chama kina taratibu zake na miongozo yake, ukigombea sio lazima jina lako lirudi, ndio maana kuna vikao vya mchujo’’ Alisema
Alisema kuwa mtu ambaye hakuteuliwa akisusia chama  hafai kuwa kiongozi na kwamba kiongozi aliyekomaa kisiasa  hapaswi kususia chama na badala yake hujipanga katika chaguzi zingine.
‘’ Mfano mzuri huu hapa kwa Abood, mwaka 2000 Abood aligombea ubunge lakini katika mchakato huo  wagombe wote walifutwa na kutangazwa upya nafasi hiyo lakini hakununa na sasa amepata ubunge’’ Alisema
Alisema kuwa uongozi hupagwa na Mungu na kwamba kama hukuchaguliwa kwa sasa jua wakati wako bado na ukifika utakuwa kiongozi tu.
Kwa upande mwingine Mangula aliwasisitiza wanachama wa CCM kudumisha ujamaa kwani ndio unaowaunganisha watanzania.
‘’ Watu wengu hudhania kuwa ujamaa umepitwa na wakati lakini hawajui kuwa ujamaa ndio unatuunganisha sisi watanzania’’ Alisema
Alisema kuwa Siasa za chuki na vurugu hazina mashiko na badala yake viongozi wazuri hupatikana kwa kunadi sera .
Mkoa wa Morogoro uliingia katika uchaguzi mdogo wa udiwani baada ya madiwani wake wa CCM katika kata ya Tungi na Rudewa wilayani Kilosa kufariki Dunia huku kata ya Kibaoni wilayani Kirombelo kubakia wazi hadi sasa kutokana na kutopangiwa kufanyika uchaguzi ambapo napo diwani wake alifariki dunia.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...