Jumatano, 5 Februari 2014

MANISPAA MORO YATEKELEZA ILANI YA CCM KWA ASILIMI 90

MEYA wa manispaa ya Morogoro Amiri Nondo amesema kuwa manispaa hiyo imefanikiwa kutekelza ilani ya uchaguzi ya chama cha Mapinduzi CCM kwa asilimi 90.

Meya huyo alisema hayo jana wakati akizungumza katika kikao maalumu cha kupokea taarifa za utekelezaji wa ilani kwa madiani wa halmashauri hiyo.
Alisema kuwa utekelezaji huo umefanyika katika kila sekta ikiwemo elimu, afya, masoko, maji, utawala bora na mengineyo.
Alisema kuwa kwa upande wa afya manispaa hiyo tayari imeshaanza ujenzi wa hospitali ya wilaya ambayo hadi sasa imeshanza ujenzi wake na inatarajiwa kuanza kutumika mapema mwezi ujao kwa huduma za nje.
Hata hivyo alisema kuwa hadi sasa kata 22 kati ya 29 zinavituo vya afya huku zingine zikiendela na ujenzi lengo likiwa ni kusogeza huduma hiyo karibu na kuepuka msongamano katika zahanati na hospitali ya rufaa ya mkoa.
Pia alisema kuwa kwa upande wa elimu walifanikiwa kujenga shule za kata 23 kati ya kata 29 na kwamba kwa sasa wanafunzi wote wanaofaulu wanapata fulsa ya kuanza masomo mapema.
Alisema kuwa halmashauri hiyo inaendelea kufanya utamini wa majengo ili kuanzisha utaratibu wa wenye majengo kulipia kodi zao katika benk na kuepuka usumbufu wa kulipia katika halmashauri hiyo.
Mwisho

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...