MAKAMO Mwenyekiti wa
chama cha Mapinduzi Taifa Philipo Mangula amesema kuwa muda wa kampeni za Urais,udiwani, ubunge na hata nafasi za
serikali za mitaa bado na kwamba
wanaofanya kampeni wanakiuka katiba na kanuni na hivyo CCM inatambua mitandao yote na
itawashughulikia.
Alisema hayo Februari 8 mwaka huu wakati akiongea na
viongozi wa wilaya na mkoa wa Morogoro alipofika kwajili ya kampeni za Uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata za Ludewa wilayani
Kilosa na Tungi Manispaa ya Morogoro.
Alisema kuwa tayari walishafungua mafaili ya watu hao wenye
mitandao ya kampeni na kwamba wanatambua mitandao yote hata katika ngazi za
mikoa na watawashughulikia.
Alisema kuwa Rais, wabunge na madiwani waliopo
madarakani bajeti yao ya mwisho inashia mwezi Juni 2015 na kwamba wanaojitokeza sasa ni waharifu na
lazima wachukuliwe hatua.
Aidha alisema kuwa Viongozi
waliopo madarakani wanahaki zote na kwamba ni lazima walindwe ili waweze
kufanya kazi zao vizuri bila kunyanyasika na kwamba kuanza kampeni hizo
kunafanya kuwavunja nguvu viongozi hao.
‘’Mara zote tatizo la kuanzisha
makundi kabla ya kampeni ni kusababisha chuki na uhasama na kupelekea makundi
hayo kurushiana maneno, na hiyo inasababisha hata nchi kushindwa kutaalika’’
Alisema
Aliwataka viongozi kutengeneza
mitandao ya kuwafutilia watu hao wenyekufanya kampeni za chini kwa chini
kinyume na taratibu na kukabiliana nazo .
‘’ Ni mwiko kwa mtu kuunda vikundi
na kufanya kampeni za chini kwa chini , tutakabiliana nazo’’ alisema.
Alisema kuwa suala la kutangaza
nia ya kutaka kugombea nafasi yeyote sio kosa bali kuanza kampeni ndio kosa
kubwa kimaadili ya chama.
Kwa upande mwingine Mangula
alisema kuwa wabunge na madiwani kufanya zaira za mara kwa mara ni sawa na
mkulima kupalilia shamba lake hivyo wanaodharau kufanya hivyo wasije kulaumu na
kwamba watavuna walichopanda.
‘’ Ni dhambi kubwa kwa mbunge kutotekeleza ahadi zake, ni sawa na mkulima kupanda mbegu pasipo
kufanya palizi, akikuta mazao yake yameliwa na magugu atamlaumu nani’’ Alisema.
Kwa upande mwingne Mangula alisema
kuwa nia ya mwenyekiti wa CCm taifa Rais jakaya Kikwete ni kuhakikisha katiba
inakamilika haraka ili itumike katika
uchaguzi ujao.
Alisema kuwa itakuwa vema ndani ya
siku 70 zilizopangwa kwaajili ya bunge la katiba ikakamilika na kurejeshwa kwa
wananchi ili kutimiza malengo
yaliokusudiwa.
Awali katibu wa CCM mkoa wa
Morogoro Rojas Romuli alisema kuwa wapo baadhi ya viongozi walionuna baada ya
majina walioyataka kurejeshwa katika uchaguzi huo kutorudi na hivyo kususia
kampeni jambo ambalo Mangula alisema
kuwa si dhambi kurejeshwa kwa mgombe wa nafasi ya 3 kinachozingatiwa ni vigezo.
Pia alisema kuwa katika kata ya
Ludewa wananchi wake wanalalamikia mbunge wao Mustapha Mkulo kutotimiza ahadi
alizoahidi.
Makamo mwenyekiti wa CCm Taifa Philipo Mangula akivishwa skafu na
chipukizi baada ya kuwasili katika ofisi za CCM mkoa wa Morogoro.
Makamo mwenyekiti huyo akisalimiana na mjumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wa Morogoro Juliana Mwenda.
makamo huyo akisalimiana na katibu wa UVCCM mkoa wa Morogoro Nicodemas.
Makamo huyo akiongea na baadhi ya viongozi wa CCM mkoa wa Morogoro pamoja na wa wilaya ya Morogoro mjini.
Hayo ni mapokezi aliopata alipoingia katika kata ya Rudewa wilaya ya Kilosa
Mangula akifungua shina la wakereketwa la Njia panda katika kata hiyo ya Rudewa
Maelfu waliofurika katika kata hiyo wakati wa kampeni ya udiwani ya Rudewa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni