Waziri wa nchi ofisi ya
Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa Hawa Ghasia akioongea na wajumbe wa baraza la wizara hiyo wakati wa kujadili bajeti ya wizara yake uliofayika jana mjini hapa
Baadhi ya wajumbe wa baraza hilo wakisikiliza kwa makini mkutano huo wa baraza jana
Wajumbe wa baraza hilo .
Habari zaido soma hapo chini
Waziri wa nchi ofisi ya
Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa Hawa Ghasia amesema upangaji wa vituo kwa watumishi wapya hususani
walimu ni eneo moja wapo lenye hafuru ya Rushwa
na kutaka watumishi wanaotuhumiwa kuchukuliwa hatua.
Alisema eneo hilo limeanza
kutoa dalili si njema na kuongeza kuwa ni vyema wakachukua tahadhari na
kujiridhisha kwa kubaini mapungufu ya kiutendaji katika eneo hilo na
kuhakikisha wanaziba mianya ya rushwa.
Alisema hayo Mei 5 mwaka huu
wakati akifungua baraza la wafanyakazi wa ofisi ya waziri mkuu Tawala za mikoa
TAMISEMI linaoendela mkoani Morogoro.
Aidha alimuagiza katibu mkuu
wa wizara hiyo kuchukua hatua za haraka dhidi ya watumishi
wanaotumiwa kwa rushwa au kutoa huduma kwa upendeleo na wale wanaoshirikiana na
maafisa katika mamlaka za serikali za mitaa kuzihujumu mamlaka hizo.
Waziri Ghasia alisema ofisi
hiyo imepigiwa kelele kwa muda mrefu na wadau mbalimbali juu ya vitendo
vya rushwa,hivyo ni wakati sasa kwa wizara hiyo kuchukua hatua madhubuti za
kuboresha mifumo ya
‘’ Ni muda muafaka sasa kuhakikisha tuhuma hizo zinakwisha,
kwa kuchukua hatua madhubuti za kuborsha mifumo ya utendaji kazi katika eneo
hili’’ Alisema
Alisisitiza juu ya kuimarisha usimamizi na ufutiliaji wa
matumizi ya fedha kupitia MSM kupitia mifumo ya fedha waliokwishawekeza
(Epcor/IFMS) ambapo alisema dalili zinaashiria ufuatiliaji kupitia mifumo hiyo
bado ni hafifu.
Katibu mkuu Ofisi ya waziri
mkuu TAMISEMI Jumanne Sagini aliwataka watumishi wa ofisi hiyo
kujadili changamoto zinazoikabili ofisi hiyo ili ziweze
kutatuliwa na waweze kufanya kazi kwa ufanisi.
Kikao cha baraza la wafanyakazi
ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa kinafanyika mjini
Morogoro na kimelenga kujadili bajeti ya wizara hiyo kabla ya kwenda kujadiliwa
kwenye bunge la bajeti mjini Dodoma.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni