January Makamba kushoto akizungumza na baadhi ya wananchi wake jimboni Bumbuli hivi karibuni.
MBUNGE
wa Bumbuli kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), January Makamba,
ameelezea kusikitishwa kwake na masuala ya imani ya kishirikina kupiga
hodi kwenye Jimbo lake.
Alisema
kuwa baada ya kuona hivyo, aliamua kuzungumza na viongozi na Mkuu wa
Wilaya kwamba watu hao wafukuzwe mara moja na wakamatwe kwasababu zoezi
hilo ni kinyume cha Sheria za nchi.
"Vilevile, katika zama hizi mambo ya uchawi na kutafuta wachawi hayana nafasi kabisa. Ni mambo ambayo yametubakiza nyuma kimaendeleo miaka nenda rudi.
"Baada
ya witch-hunters kufukuzwa kuna baadhi ya vijana walioratibu ujio wao
walienda kituo cha polisi Bumbuli na kujaribu kung'oa dirisha na kuvunja
mlango. Kituo cha Polisi hakijachomwa moto. Pia wakaenda kwenye Ofisi
ya Afisa Tarafa na kujaribu kuvunja Ofisi," alisema Makamba.
Aliendelea
kusema kuwa wote wamekatwa Jumapili na kupata message nyingi za wapiga
kura wakimpongeza kwa kuzuia upuuzi na wengine wakitaka waruhusiwe watoa
uchawi.
"Kama viongozi, tunayo kazi kubwa ya kuelimisha watu kuhusu hizi imani.
Changamoto
kwetu kule sio tu masuala ya barabara, maji, umeme, nk lakini pia haya
masuala. Bahati mbaya imani za kichawi zimeshamiri sana kwenye jamii
nyingi za Kiafrika na kazi ya kuziondoa ni kubwa sana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni