Jumatatu, 22 Aprili 2013

MATUKIO MBALI MBALI YA HITIMISHO YA ZIARA YA KINANA MKOA WA MOROGORO

Katibu Mkuu wa CCM akisalimiana na wakazi wa kata ya Kirongo wakati wa ufunguzi wa kisima cha maji Mkoani Morogoro.



Moja ya Visima Kumi vilivyokamilika ambavyo vipo kwenye mradi wa visima 23 vinavyojengwa kwa gharama  shilingi milioni mia tatu na sitini elfu.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya ufunguzi wa kisima cha maji kata ya Kirongo,mkoani Morogoro.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Andulrahman Kinana  akimtwisha ndoo ya maji mwana mama wa kata ya Kirongo,baada ya ufunguzi wa kisima cha maji.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wazee wa shina no.2,kata ya Mwembesongo.


Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea zawadi ya muwa shina no.2,kata ya Mwembesongo.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa na nyuso ya furaha baada ya kupokelewa vizuri na wananchi wa kata ya Mwembesongo,Morogoro. 

Katibu Mkuu wa CCM,ndugu Andulrahman Kinana akihutubia wananchi wa shina no. 2 kata ya Mwembesongo, ambapo pamoja na kufungua shina hilo la umoja wa wazazi pia alifanya harambee iliyofikia kiasi cha shilingi milioni mbili ,ambazo zitatuika kama mtaji wa shina hilo linalojishughulisha na shughuli za ujasiriamali wa kutengeneza sabuni na mamashughuli za mama lishe.



Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wakiwasili kwenye mkutano wa hadhara ,kwenye viwanja vya Shule ya msingi Kiwanja cha Ndege,Morogoro.

Msanii Linah akitumbuiza wananchi wa Morogoro waliokuja kwenye mkutano wa CCM.

Wasanii wa Wanaume Family wakitumbuiza wananchi wa mkoa wa Morogoro wakati wa mkutano wa hadhara wa CCM.

Msanii Diamond akitumbuiza wakazi wa mkoa wa Morogoro wakati wa mkutano wa CCM katika viwanja vya shule ya msingi Kiwanja cha Ndege,Morogoro.

Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi akihutubia mamia ya wakazi wa Morogoro kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya msingi Kiwanja cha Ndege.

Robert F. Selasela Diwani wa Kata ya Kiloka akisalimia wananchi waliokuja kwenye mkutano wa CCM, Robet ni mmoja wa Viongozi vijana  walio ndani ya CCM.


Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia umati mkubwa uliokusanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kiwanja Cha Ndege,Morogoro.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...