Jumanne, 23 Aprili 2013

Rais Kikwete amemteua Bi. Juliet Kairuki kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bibi Juliet Rugeiyamu Kairuki kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).
Taarifa iliyotolewa jana, Jumatatu, 22 Aprili, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, inasema kuwa uteuzi huo ulianza Aprili 12, mwaka huu, 2013.
Bibi Kairuki ni Mwanasheria mwenye Shahada ya Kwanza na ya Uzamili kwenye sheria. Ni mtaalam wa miradi ya ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi (Public Private Partnership). Kati ya mwaka 2002 na 2008 alikuwa Meneja wa Mradi wa Public Private Partnership Capacity Building in SADC, katika Chama cha Mabenki ya Afrika Kusini (The Banking Association South Africa). Kuanzia mwaka 2008 hadi sasa Bibi Kairuki ni Meneja Mkuu wa Idara ya Benki na Huduma za Fedha katika taasisi hiyo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
DAR ES SALAAM.
22 Aprili, 2013

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...