Baadhi ya wafanyakazi wa Manispaa ya Dodoma wakifurahia wakati wa kilele
cha Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), Mjini Dodoma jana. Picha na
Edwin Mjwahuzi.
MBEYA.
RAIS Jakaya Kikwete ametangaza neema kwa
wafanyakazi baada ya kuahidi kuwa Serikali itawapunguzia makato ya kodi
(Paye) na pia itawaongezea mishahara.
Akihutubia taifa katika kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) mjini Mbeya jana, Rais Kikwete alisema Serikali imeitikia kilio cha muda mrefu cha wafanyakazi.
Akihutubia taifa katika kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) mjini Mbeya jana, Rais Kikwete alisema Serikali imeitikia kilio cha muda mrefu cha wafanyakazi.
Aliahidi kuwa Serikali itatangaza punguzo hilo la
ongezeko la kodi na mishahara kwa watumishi wa umma wakati Waziri wa
Fedha, Dk William Mgimwa atakapowasilisha Baj
eti ya Serikali ya Mwaka
wa Fedha wa 2013/14.
Pia alisema Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia
Kabaka atatangaza nyongeza ya mshahara kwa sekta binafsi
atakapowasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake.
Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa Serikali
kupunguza kodi hiyo kwani mwaka 2007, iliipunguza kutoka asilimia 18
hadi 15 na mwaka 2010 iliipunguza tena hadi asilimia 14.
Rais Kikwete alisema mfumo wa makato ya kodi
unatokana na kipato cha mtu jambo ambalo limechangia wengine kukatwa
kiasi kikubwa na wengine kidogo lakini akasema anaamini kuwa makato hayo
yataendelea kupungua bila ya kuathiri uchumi wa nchi.
Mishahara
Rais Kikwete alisema kuwa katika bajeti hiyo, Serikali itatangaza nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma na sekta binafsi huku akiahidi kuwa italingana na hali halisi ya maisha.
Alisema kutokana na hali hiyo, Serikali imetenga zaidi ya Sh4.76 trilioni katika Bajeti ya Mwaka 2013/14 kwa ajili ya mishahara ya wafanyakazi wa umma.

Alisema katika Bajeti hiyo, asilimia 44.9 ya fedha
itakuwa kwa ajili ya mishahara ya wafanyakazi, fedha ambazo zitatoka
katika vyanzo vya mapato vya ndani.
Alisema katika kiasi hicho, zaidi ya asilimia 4.9 zinatoka kwenye mapato ya Serikali na kilichobaki kitatoka kwenye vyanzo mbalimbali.
Alisema katika kiasi hicho, zaidi ya asilimia 4.9 zinatoka kwenye mapato ya Serikali na kilichobaki kitatoka kwenye vyanzo mbalimbali.
“Tunajua kuwa, mishahara ya wafanyakazi ni midogo,
lakini Serikali imekuwa ikijitahidi kuongeza kila mwaka ili iweze
kuendana na hali halisi ya maisha,” alisema.
Alisema mwaka juzi, kima cha chini kilikuwa Sh65,000 ambacho kiliongezwa hadi kufikia Sh125,000 na kwamba mwaka huu wataongeza kiasi kikubwa ili kiweze kukidhi mahitaji.
Alisema mwaka juzi, kima cha chini kilikuwa Sh65,000 ambacho kiliongezwa hadi kufikia Sh125,000 na kwamba mwaka huu wataongeza kiasi kikubwa ili kiweze kukidhi mahitaji.
Mifuko ya Jamii
Akizungumzia kuhusu Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Rais Kikwete aliwaondoa hofu wananchi na kusema iko hai na wafanyakazi watakaostaafu watalipwa mafao yao kama kawaida.
Alisema utafiti uliofanywa hivi karibuni na Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), umebaini kuwa mifuko hiyo haina matatizo yoyote.

Alisema Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma
(PSPF), ulikuwa na matatizo ambayo yalianza kabla ya mwaka 1999, jambo
ambalo lilifanya uwe na madeni ya zaidi ya Sh6 trilioni. Baada ya kuona
hivyo, alisema Serikali iliweka utaratibu wa kuuchangia kiasi cha Sh50
bilioni kila mwaka katika mapato yake.
Alisema kutokana na hali hiyo fedha hizo ndizo
zinazotumika kulipa wafanyakazi na wastaafu mafao yao na kwamba mpaka
sasa hakuna aliyelalamika kutolipwa mafao yake.
“Naomba niwaondoe hofu Watanzania wenzangu. Hakuna
mfanyakazi atakayekosa kulipwa mafao yake pindi anapostaafu katika
mifuko ya hifadhi ya jamii ukiwemo PSPF,” alisema Rais Kikwete na
kuongeza kuwa uwekezaji katika mifuko hiyo unakua siku hadi siku.
Rais Kikwete aliwashauri waajiri kuwaacha wafanyakazi wajiunge na mfuko wowote wanaotaka ili waweze kuhifadhi mafao yao.
Rais Kikwete aliwashauri waajiri kuwaacha wafanyakazi wajiunge na mfuko wowote wanaotaka ili waweze kuhifadhi mafao yao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni