
Mwenyekiti wa TACAIDS Dk. Fatma
Mrisho (katikati) akizungumza wakati kufungua warsha siku moja ya
mapitio na uhakikisho wa Ripoti ya hali ya Elimu na Huduma za Afya ya
uzazi, maadili na mahusiano ya kingono kwa Vijana nchini ambapo
warsha hiyo imeshirikisha Taasisi mbalimbali zikiwemo AMREF, UNICEF,
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kutoka Tanzania Bara na Visiwani,
TGNP, Wizara ya Afya na ustawi wa Jamii na nyinginezo. Kushoto ni Abdoul
Coulibaly wa UNESCO na kulia ni Mwezeshaji wa Warsha hiyo kutoka Chuo
kishirikishi cha Elimu cha Chuo kikuu cha Dar es Salaam (DUCE) Dr.
Kitila Mkumbo.
Mwezeshaji
wa Warsha hiyo kutoka Chuo kishirikishi cha Elimu cha Chuo kikuu cha
Dar es Salaam (DUCE) Dr. Kitila Mkumbo akitoa mwongozo kwa washiriki wa
warsha hiyo ambapo katika majumuisho yalioamuliwa kwenye warsha
iliyofanyika leo ya kujadili Ripoti ya hali ya Elimu na Huduma za Afya ya uzazi, maadili na mahusiano ya kingono kwa Vijana nchini yatawasilishwa katika mkutano wa Mawaziri utakaohusisha nchi 21 za Afrika Mashariki na Kusini.
Picha juu na chini ni National
Program Officer – HIV & Sexuality Education Mathias Herman kutoka
UNESCO akichambua mpango wa majukumu ya nchi za Afrika Mashariki na
Kusini na kutoa ufafanuzi wa matokeo ya utafiti wa Ripoti ya hali ya Elimu na Huduma za Afya ya uzazi, maadili na mahusiano ya kingono kwa Vijana nchini ambapo
ameongeza kuwa nchi inatakiwa kujipanga kwa kusaidiwa na UNESCO pamoja
na washirika kuongoza jitihada za kitaifa ambazo zitawawezesha washirika
wakubwa ambao ni vijana kushiriki katika mikakati ya kitaifa
itakayowasidia vijana nchini kujua mtazamo wao.
Pichani ni Washirki wakifuatilia uchambuzi wa Ripoti uliokuwa ukiwasilishwa na Mathais Herman kutoka UNESCO.

Mwakilishi kutoka Wizara ya Elimu na Ufundi stadi Bw. Raymond Benedict (kushoto) akikata kujua kuhusu mapitio ya Ripoti ya hali ya Elimu na Huduma za Afya ya uzazi, maadili na mahusiano ya kingono kwa Vijana nchini, huduma zinazotolewa na serikali na nini hatma na vijana wameelewa kwa kiwango gani.
Pichani juu na chini washiriki
wa warsha ya siku moja iliyoandaliwa na shirika la UNESCO nchini
wakichangia maoni yao.Pichani juu Katikati ni Mwenyekiti wa Asasi ya
vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA) Lwidiko Edward akiwakilisha vijana na
kulia ni Abdoul Coulibaly wa UNESCO
Picha juu na chini ni Washirki
wakiendelea kufuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye warsha ya siku moja ya
ya mapitio na uhakikisho wa Ripoti ya hali ya Elimu na Huduma za Afya ya uzazi, maadili na mahusiano ya kingono kwa Vijana nchini iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam na kufunguliwa na Mwenyekiti wa TACAIDS Dk. Fatma Mrisho.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni