NAIBU Waziri  w a elimu ya juu  nchini Afrika Kusini Mduduzi Manana jana  amejikuta katika mazingira magumu  baada ya vijana walioachwa na wapigania uhuru pamoja na wakimbizi wa nchi hiyo, kumvaa na kutaka kuwapa majibu ya hatima yao juu ya suala la elimu.
Sintofahamu hiyo ilimkuta waziri huyo wakati alipokuwa akitembelea eneo kilipokuwa chuo cha wapigania uhuru wa Afrika  kusini cha Solomoni Mahalangu (SOMAFCO) ambacho sasa ni kampasi ya chuo kikuu cha kilimo SUA.

Mery Twala ni mmoja wa watoto kati ya 80 walioachwa na wakimbizi hao waliokuwa wakiishi Mazimbi manispaa ya Morogoro, ambao  kwa sasa wanaishi eneo la Dark Cite pamoja na mama zao  ambapo wengine wamefiwa na wazazi wao wote wawili.

‘’Tumechoka ,mnakuja na kutulisha chakula  tuu bila kuelewa hatima yetu katika elimu’’ alisema kwa sauti ya juu mtoto huyo.
Alisema   wao walizaliwa watatu na kwamba baada ya kupatikana kwa uhuru wan chi hiyo baba yao aliondoka na kaka na dada yake huku akimwacha yeye na mama yake ambaye kwa sasa ameshafariki dunia.

Alisema ameshindwa kupata elimu sahihi kutokana na mazingira magumu kwani mama zao walikuwa wafanyakazi wa ndani wa wapigania uhuru hao hivyo baada ya kuondoka kazi na masomo ya watoto hao havikuendelea.

 ‘’ Mimi siwaelewi hawa watu kila mwaka wanakuja lakini hawatutatulii matatizo yetu, wanajua baba zetu waliondoka na kutuacha tunasoma lakini tuliachishwa na na kushindwa kuendelea na shule,, alisema
Vijana hao kwa pamoja waliitaka Serikali hiyo  kutoa tamko rasmi kama haiwatambui  ili wajue  kuwa wao ni watoto wa mitaani na yatima.

Kilio cha vijana hao kilimgusa waziri huyo na kusema Serikali yake haita kaa kimya na itahakikisha inatatua tatizo hilo kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania.

Hata hivyo Naibu waziri huyo alisema ugeni huo haukuja kwa masula hayo  na kwamba kutoa majibu ya moja kwa moja itakuwa ngumu kwake na kuahidi kulifikisha suala hilo mara atakapurudi nchini kwao.

Naye Anna Mngoni aliishushia lawama serikali hiyo kwamba waliwaahidi  baada ya kupata uhuru watarudi ili kuja kuwalipa mafao ya wastaafu lakini hadi sasa ni miaka 20 imepita hakuna mwelekeo wowote.

‘’ Mimi ni mstaafu wa ANC, walipoondoka tulistaafishwa kazi, lakini hadi sasa hatujalipwa, wenzetu wengine walishakufa, nasie  ni wafu watarajiwa, tunataka kujua hatma  ya malipo yetu’’ alisema.

Hata hivyo Waziri huyo alisema kwa kuwa serikali hiyo iliahidi suala hilo ni lazima lishughulikiwe na kuwataka kuvuta subira ili nalo aweze kuliwasilisha  ili kuweza kutolea majibu sahihi.
Naibu waziri huyo kabla ya kuongea na wanajumuiya ya SUA , mamia ya wanachama  wa Chama cha Mapinduzi CCM , na watoto hao alitembelea makaburi ya wapigania uhuru na wakimbizi katika kampasi  ya mazimbu na kuweka mashada.

 Afrika kusini inatimiza miaka 20 tangu kupata uhuru wa Kidemokrasia, imeamua kuleta vijana 30 kutoka vyuo vikuu vya nchi hiyo kutembele mazimbu moro  ili kujua historia ya nchi yao.