Jumapili, 10 Agosti 2014

MGOGORO WA ARDHI WAZUKA TENA MVOMERO, VITISHO VYATAWALA , WANANCHI WAPORWA MASHAMBA NA KUPEWA VIGOGO

Michael Mayalla mwenyekiti kitongoji cha Majichumvi akiongea katika mkutano wa pamoja na wananchi wa kitongoji hicho, waliokutana kujadili  madai ya kuporwa mashamba yao yanayodaiwa kupewa vigogo.
Mwananchi huyo alikutwa aneo hilo la maji Chumvi akiteka maji , ambapo alidai kuna changamoto ya maji sambamba na uchafuzi wa maji hayo unaofanywa na wafugaji,
Habari zaidi soma hapo chini,
KUMEZUKA  Mgogoro mkubwa  katika kitongoji cha  Majichumvi kijiji cha Wami Luhindo  wilayani  Mvomero  kufuatia maafisa ardhi kuanza zoezi la  upimaji  na  ukaguzi wa mashamba pori yaliyotekelezwa zaidi ya miaka 30  na wamiliki halali wa mashamba hayo.

 Mgogoro unatokana na maafisa ardhi kuanza zoezi hilo zaidi ya mwezi mmoja sasa bila kutoa taarifa ama  elimu yoyote kwa uongozi wa kijiji hicho juu  ya nini wanachofanya.

Michael Mayalla mwenyekiti kitongoji cha Majichumvi alisema hayo  juzi wakati wa mkutano  wa pamoja  na wananchi wa kitongoji hicho waliota kujua hatma yao juu ya mashamba hayo.

‘’Tunashangaa kuona  watu wa ardhi wanakuja kupima mashamba yetu huku  wakijua kuna wakulima na wafugaji walihamishiwa  humo  kwa zaidi ya miako 10 iliyopita’’alisema

Mwenyekiti huyo alisema maafisa hao wa ardhi wakiulizwa juu ya suala hilo wamekuwa wakitoa kauli za vitisho  kwa  wakazi hao , wakidai   mashamba hayo yanamilikiwa na vigogo.

Afisa ardhi wa wilaya ya Mvomero Majaliwa Jafari alisema kati mwaka 1980 hadi 1990 serikali ilitenga ekari 60,000 za mashamba  kwa ajiri ya kilimo cha nguvu kazi katika kijiji hicho.

Hata hivyo alisema baadhi ya mashamba  yalinunuliwa na baadhi ya  watu  ambapo mengi hawakuendelezwa.

Alisema kutokana na hali hiyo serikali ilitoa agizo kuyatambua mashamba pori ili yaweze kufutwa na kuangalia nini cha kufanya.

 Mgogoro unajitokeza ,ni sitofahamu kwa  wananchi waliohamishiwa humo na wanaoishi zaidi ya miaka 10 sasa ambao  ni wakulima na wafugaji zaidi ya 1000 baada ya serikali kuanza zoezi la ukaguzi  na upimaji wa mashamba hayo bila taarifa kwao.

Mwenyekiti wa kijiji cha Wami Luhindo Apolinali Kahumba anasema katika kijiji chake kuna vitongoji 6 ambapo Maji chumvi ni miongoni mwa vitongoji hivyo.

Alisema kinachofanyika ni Halmashauri kutowashirikisha kama uongozi wa kijiji na kwamba hata pale walipopeleka maombi yao ili waweze kujua ni eneo lipi ambao wananchi wanapaswa kutumia kumekuwa hakina majibu sahihi.

Alisema  kwa mujibu wa sheria vijiji  vina mamlaka ya kugawa eneo lake kupitia mkutano mkuu wa kijiji  na kwamba kama serikali inahitaji eneo ni lazima kijiji kishirikishwe

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...