Ijumaa, 10 Mei 2013

WAUGUZI KUADHIMISHA SIKU YAO UDSM, WANANCHI WAASWA KUHUDHURIA

9,mama salma kikwete akisalimiana na wauguzi wa kituo cha afya Butiama- Okt,12,2011
Na Frank Shija – MAELEZO
Wananchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujitokeza katika maadhimisho ya siku ya wauguzi dunia itakayofanyika kimkoa katika viwanjwa vya chuo kikuu cha Dar es Salaam, kuanzia siku ya Jumamosi tarehe 11 na kufikia kilele tarehe 12 mei 2013.
 Wito huo umetolewa  na mwakilishi wa chama cha wauguzi tawi la mkoa wa Dar es Salaam Bi. Joan Bigirwa  alipokuwa akiongea na waandishi wahabari leo (jana) jijini Dar es Salaam.
 Joan alisema kuwa kutokana na kaulimbiu ya mwaka huu kuhusu malengo ya millennia yanahusu vijana wameamua kufanyia maadhimisho hayo katika viwanjwa vya chuo kikuu ili kutoa fursa kwa vijana wengi kushiriki katika maadhimisho hayo.
 Aidha amesema kwamba maadhimisho hayo yanataraji kuanza saa tatu asubuhu kwa maandamano kututoka Ubungo hadi viwanja vya Chuo Kikuu cha  na kupokelewa na mgeni rasmi ambaye atakuwa ni Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam.

 Naye Mwenyekiti wa TANNA tawi la vyuo vikuu Bi. Wilhelmina R. Niwabigira ameongeza kuwa maadhimisho hayo yataambatana na utoaji wa huduma mbalimbali.
Niwabigira ametaja baadhi ya huduma hizo zitakazotolewa ni ushauri nasaha,kupima saratani ya shingo ya kizazi na matiti,kupima kisukari,afya ya akili, presha na ushauri wa vicoba ambapo huduma zote zitatolewa bure.
 Siku ya wauguzi dunia usherehekewa kila mwaka kwa kumkumbaka mwanzilishi wa uuguzi nchini Bi. Florence Nightngale.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...