Kurasa
HOME
UVCCM
UWT
WAZAZI
WABUNGE
MAWASILANO
WAASISI/CCM
VIONGOZI MORO
Jumamosi, 1 Juni 2013
ABDULRAHMAN KINANA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI WANGING’OMBE
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Wangamiko Kata ya Malangali Wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe jana wakati alipotembelea mradi wa ufugaji wa nyuki unaoendeshwa na jumuiya ya wa Wazazi ya CCM wilaya ya Wanging’ombe mkoani humo, Pia Kinana aliridhishwa na shughuli za maendeleo zinazofanywa na vijana wa kitongoji hicho na kuamua kuwapatia jumla ya shilingi milioni 10 ili kujiendeleza katika shughuli zao za miradi ya kiuchumi , pia aliwapatia jezi za michezo seti mbili na mipira 10 kwa ajili ya kuunda timu zao za mpira wa miguu
. Katika hatua nyingine alikipa kitongoji hicho mifuko 25 ya saruji ili kumalizia ofisi yao ya CCM, Katika maombi yao wananchi hao wamemuomba Katibu Mkuu wa (
CCM) kulifikisha ombi lao kwa TAMISEMI ili kitongoji hicho kipandishwe na kuwa na hadhi ya kijijiPICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-WANGINGOMBE-NJOMBE
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abulrahman Kinana akizindua mradi wa ufugaji nyuki katika kitongoji cha Wangamilo kwa kuutundika mzinga wa nyuki kwenye mti, mradi huo unaedeshwa na jumuiya ya wazazi ya CCM Wilaya ya Wanging’ombe, Kinana aliipatia jumuiya hiyo mizinga mingine 25 ili kuendeleza mradi wao
Umati wa wananchi ukinyanyua mikono juu kuashiria kufurahishwa na hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana hayupo pichani
Katibu wa Itikadi , Siasa na Uenezi CCM Nape Nnauye akimpiga picha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana wakati alipokuwa akihutubia katika kitongoji cha Wangamiko
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahmani Kinana na Katibu Wa Itikadi , Siasa na Uenezi Nape Nnauye waakichanganya Mchanga na saruji wakati walipotembelea na kukagua ujenzi wa zahanati ya Samaria Wangingombe
Hapa akikagua ujenzi wa Zatanati ya Samaria na kuuliza maswali kadhaa, hata hivyo aliridhishwa kwa mjinsi wananchi wanavhoshiriki shughuli za maendeleo katika kata hiyo.
Hapa akiangalia unga wa mahindi unaotengenezwa na Kiwanada cha Mbomole Investiment Co. Cha Malangali Wanging’ombe wakati alipotembelea maonyesho ya wajasiriamali na wakulima wilayani humo
Hapa akizungumza na wananchama wa shina moja wapo katika kata ya Iwawa Makete shina hili linaongozwa na mzee Danke Sanga
Abdulrahman Kinana akilakiwa na wananchi mbalimbali wakati akiwa njiani kuelekea Wilaya ya Wanging’ombe
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki zoezi la kufyatua tofari wakati alipotembelea ujenzi wa zahanati ya Samaria akiwa njiani kuelekea Malangali Wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Chapisho Jipya
Taarifa za zamani
Nyumbani
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni