Jumatatu, 24 Juni 2013

TASO KUANZISHA SACCOS YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

MAKSAINa Gladness Mushi, Arusha
Chama cha wakulima na wafugaji kanda ya kaskazini(TASO)kinatarajia kuazisha chama cha kuweka na kukopa (SACCOS)kwa ajili ya kuwasaidia wanachama wake kwani mpaka sasa uzoefiunaonesha kuwa baadhi ya
wakulima na wafugaji wadogo hawapewi mikopo na taasisi za fedha.
Hayo yameelezwa mapema jana na Katibu mkuu wa chama hicho,Bw Peter Ngasa wakati akiongea kwenye kikao cha wazi kilichojumuisha wanachama na wadau wote wa chama hicho.
Ngasa alisema kuwa kuwepo kwa Saccos hiyo kutaweza kuruhusu maendeleo makubwa ya wakulima pamoja na wafugaji wa kanda hiyo kwani wengi wanakosa mahitaji muhimu kutokana na kuwa hawaaminiki na taasisi za mikopo.
Aliongeza kuwa kupitia Saccos hiyo waraweza hta kukopa hadi vifaa vya kilimo kama vile pembejeo za kilimo na kulipa kwa wakati hivyo basi hata kilimo cha kanda ya kaskazini nacho kitaweza kuimarika zaidi
“Tafiti ambazo nimezifanya mimi nimegundua kuwa hili kundi la wakulima na wafugaji wadogowadogo ndilo kundi ambalo linasahulika sana na hata mabenki wakati mwingine yanashimndwa kutoa mikopo kwa kuhofia hata vifo vya wanyama au wizi sasa kama tutakuwa na chama chetu cha kuweka na kukopa basi tutaweza kuraisisha kazi na mabadiliko lazima yataonekana” aliongeza Ngasa
Wakati huo huo alisema kuwa kwa sasa TASO imejipanga kuhakikisha kuwa kila mwezi kunakuwa na mabadiliko katika sekta ya kilimo lakini hata ufugaji kwani bado kuna changamoto lukuki sana ambazo zinafanya maendeleo yaje taratibu sana
Alifafanua, mabadiliko hayo yatatokana na mbinu mbalimbali ambazo zitabuniwa na TASO ambapo mbinu hizo zitalenga kumkomboa mkulima na mfugaji kuanzia ngazi ya Kaya hadi taifa kwani uwezekano huo upo sana.
“Tunaposema kuwa tutakuwa wabunifu ni kama hivi tulivyobuni chama cha kuweka na kukopa lakini tutakuja na wazo lingine kwani matazamio yetu sisi ni kuona kuwa tunakuwa na Kilimo chenye Tija na ambacho kinalenga kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi na wala sio kilimo ambacho kinatangazwa kwenye vyombo vya habari na majarida wakati wakulima bado wanateseka”aliongeza Ngasa
Alimalizia kwa kusema kuwa nao wanachama wa TASO pamoja na wadau wa kilimo wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanabadilika na kamwe nasikubali kuingiza hata siasa kwenye kilimo,ingawaje pia wanatakiwa kuwa
wabunifu tena wa hali ya juu sana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...