Ijumaa, 25 Aprili 2014

GAZETI LA TANZANIADAIMA LAINGIA MTATANI NA WIZARA YA NISHATI NA MADINI, NI BAADA YA KUPOTOSHA HABARI

           Msemaji wa wizara ya nishati na madini Badra Masoud aliyevaa shati la drafti akinukuu masuala muhimu katika mkutano wa baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo uliofanyika mjini Morogoro kwa siku mbili Aprili 23 na 24 mwaka huu.

Habari zaidi soma hapa chini.


WIZARA ya Nishati na madini imekanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti la Tanaznia Daima la Aprili 24 mwaka huu kwamba waziri wa wizara hiyo Profesa Sospetter Muhongo amesema ni lazima watumishi wote  wakiwemo wahudumu wa wizara hiyo kuwa na kiwango cha elimu ya digrii ua udhamili jambo ambalo si sahihi.
Msemaji wa wizara hiyo Badra Masud alisema hayo jana wakati akiongea na waandishi wa habari mjini hapa baada ya kumalizika kwa baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo.
Alisema mwandishi wa habari wa gezeti hilo aliandika taarifa hizo kwa mtazamo wake na sio kwa kufuta yale yaliongelewa na waziri huyo wakati wa kufungua baraza la wafanyakazi Aprili 23 mwaka huu.
Msemaji huyo wa wizara alisema kilichongelewa na waziri ni kuwataka maafisa wa wizara hiyo kutumia fulsa za kusoma na angalao wawe na kiwango cha elimu cha digrii ya udhamili na sio kwa watumihi wote  wakiwemo wahudumu kama ilivyoandika gazeti hilo la Tanzania Daima.
Alitaka gazeti hilo kukanusha taarifa hizo kabla ya kuchukua hatua za kisheria  kutokana na kupotosha habari hiyo.
‘’ Mwandishi wa gazeti hilo alikuwa na ajenda yake na ndio maana aliandika kwa kuongeza chumvi, ni lazima waandishi wakawa makini vinginevyo wanwaweza kusababisha vyombo vyao kuingia katika matatiz  na hata  kusababisha mtafaruko na chuki katika ya jamii’’ Alisema
Wanapoandika taarifa mbalimbali wawe makini na kama hawajaelewe ni vema wakauliza na kuongeza kuwa kazi ya uandishi wa habari ni kuhabarisha na kutoa taarifa sahihi kwa jamii na sio kupotoshwa.
Badra alisema siku ya ufunguzi huo yeye mwenyewe alikuwepo na kilichoongelewa sio hicho kilichoandikwa katika gazeti hilo na kuongeza kuwa  alitoa fulsa kwa waandishi hao kuuliza masawali  na badala yake alisimama mwenyeki  wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Morogoro Ida Mushi  na kusema wameelewa na kwamba hawana maswalilabdla kwa wakati mwingine.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...