Alhamisi, 5 Desemba 2013

DIAMOND TRUST BANK WAZINDUA TAWI JIPYA MOROGORO

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Dk Joel Bendera akikata Utepe kuashiria kuzindua Tawi la Bank ya Diamond Trust Mjini Morogoro Kulia ni Meya wa Manispaa ya Morogoro Mstahiki Amiri Nondo na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo.
Meneja wa Tawi la benki hiyo Mkoa wa Morogoro Akitoa taarifa Fupi kuhusu benki hiyo ambapo katika kipindi cha miezi miwili walichokuwepo mkoani Morogoro wameweza kufungua Akaunti 2000 zawakazi wa mkoa huo.Aidha meneja huyo ameahidi kuendelea kuwahudumia wakazi wa Morogoro vizuri zaidi wa wataongeza masaa ya kufanya kazi ili kuwapa fursa wakazi wa mkoa huo kupata huduma za DTB Ipasavyo
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Dk Joel Bendera Akitoa hotuba yake Ambapo  Aliupongeza Uongozi wa benki hiyo kwa kuweka kipaumbele  katika kutoa za kibenki Kwa wafanyabiashara wadogowadogo na wajasiriamali na kufungua matawi mengi katika mikoa mbalimbali hapa nchiniikiwa ni jitihada za kupeleka huduma za kifedha kwa watu ambao hawajafikiwa na huduma za kibenki..Dk Bendera Alisisitiza Umuhimu wa Benki nyingine Kufuata Mfano ulionyeshwa na DTB ya kuelekeza jitihada katika mkupeleka huduma za Kibenki vijijini ili kutoa fursa ya kupata huduma za kibenki kwa jamii kubwa ya watanzania wasio na nafasi ya kupata huduma hiyoHilo ni tawi la 18 la benki hiyo hapa nchini

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Dk Joel Bendera akiweka saini katika kitabu cha wageni alipowasili katika benki hiyo wakati wa uzinduzi wa tawi la benki hiyo mkoani morogoro

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...