PIX17-17
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akizungumza mara baada ya kuzindua rasmi upokeaji wa mabomba ya gesi tayari kwa kusafirishwa hadi Mtwara.
PIX12-12
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akibadishana mawazo na Waziri wa Nishati na Madini Prosefa Sospeter Muhongo aliyekaa kushoto. Kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania Lu Youging wakati wa hafla ya kuzindua kupokea shehena ya mabomba kwa ajili ya mradi wa kusafirisha Gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.

PIX13-13
Mh. Mizengo Pinda akishuhudia Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Balozi Lu Youging alipokuwa akimalizia kufunua kitamba kama ishara ya uzinduzi rasmi wa upakeaji wa mabomba ya Gesi.
PIX14-14
Pichani ni mafundi wakiwa katika zoezi la kupakua mabomba kutoka katika meli na kupakia kwenye Lori tayari kwa safari ya Mtwara.
PIX1 -1
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China Balozi Lu Youging akifafanua jambo. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Prosefa Sospeter Muhongo.
PIX3-3
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Jambo Freight Forwarder Bibi Vanessa Gwau (kushoto) akielezea jambo kwa mwandishi wa habari wakati wa hafla ya kupokea mabomba yatakayotumika kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadio Dar es Salaam. Jambo Freight ndiyo kampuni iliyopewa zabuni ya kupakua shehena hiyo.
Na Frank Shija – Maelezo
Serikali imewatoa hofu wananchi wa Mtwara kuhusu kunufaika kwao na gesi asilia iliyopatikana katika maeneo yao.
Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda alipokuwa akizindua rasmi upokeaji wa shehena ya mabomba ya gesi kwa ajili ya mradi wa bomba la kusafirishia Gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
Pinda amesema kuwa wananchi wa Tanzania watanufainaka na mradi huo hasa wakazi wa Mtwara kwa kuwa vijana wengi watapata ajira wakati na baada ya kukamilika kwa ujenzi wa bomba hilo kwa kuwa viwanda mbalimbali vitajengwa mkoani Mtwara kikiwemo kiwanda cha Saruji ambacho ujenzi wake umekwisha anza.
Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Chini nchiniTanzania Lu Youging amesema kuwa Tanzania itanufaika na mradi huo, na kukua kiuchumi kwa kuwa itapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi katika nishati na badala yake itazalisha nishati yakutosha.
Balozi huyo ameongeza kuwa kupitia mradi huo Tanzania itaondokana na kuwa tegemezi katika shughuli zake za maendeleo, kwa kuwa kuna hazina ya kutosha ya gesi asilia na itawanufaisha watanzania wenyewe na si vinginevyo.
Jumla ya mabomba 3,400 yamepokelewa katika awamu ya kwanza ambapo awamu ya pili itapokelewa shehena yenye mabonmba 4,600 katika bandari ya Mtwara.
Inakadiriwa kuwa jumla ya shehena 12 zitatumika mpaka mradi utakapokuwa umekamilika.