Mkurungenzi wa makosa ya jinai wa jeshi la polisi nchini Tanzania DCI ROBERT MANUMBA amewashukuru wananchi kwa kuonesha utulivu na amani wakati wa ziara ya Rais Baraka Obama hapa nchini amesma hayo mwakati akizungumza na wandishi wa habari makao makuu ya jeshi la polisi jijini Dar es salaam leo
Aidha katika mkutano huo na waandishi wa habari Manumba amesema pia jeshi la polisi nchini limefanikiwa kukamata meno ya tembo mia tatu na arobaini na moja maeneo ya kimala jijini dsm baada ya jeshi la polisi kufanya upelelezi dhidi ya majangili wa tembo hapa nchini
Pia katika taarifa yake kwa waandishi wa wahabari dci manumba ameeleza pia kuwa jeshi la polisi linamshikili raia mmoja wa uingereza kwa tuhuma za kigaidi hapa nchini mala baada ya jeshi lapolisi kumkamata mtu huyo akiwa katika safari mpaka wa kuvuka kwenda nchini Malawi toka nchini Tanzania,
Manumba amefanuna kwamba mtuhuyo alikutwa na pasi mbili za kusafilia za Tanzania na Uingereza ambazo sio harari na zimebainika kuwa nimiongoni mwa pasi zilizo potea katika idara ya uamiaji hapa nchini.
Pia Dci amesema mala baada ya jeshi la polisi kupeleleza limebaini kuwa mtu huyo ni raia wa uingereza na alikuwa akitafutwa na serikali ya uingereza kwa tuhuma mbalimbali za kigaidi mtuhuyo mwenye asili ya kiarabu na anauraia wa Tanzania na uingereza. pia munumba amemewahadhalisha wananchi dhidi ya vitendo vya kigaidi na kusema kuwa bado vikundi vya kigaidi vipo na vinafanya matukio ya kihalifu hapa nchini na AFRIKA MASHARIKI NA DUNIA NZIMA Pia alitaja mitandao hiyo kuwa ni mtandao wa alshaababu , bokoharamu na alquider kuwa vikundi hivyo bado nihatari kwa taifa letu na afrika mashariki na dunia nzima kwa ujumla wake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni