Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kati kati ) akiwa na Mwakilishi wa Ubalozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania, Majed Al- Bagam ( kulia) pamoja na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Wariambora Nkya ( kushoto) , nyuma ( kushoto) ni Meneja wa Shirika la International Islamic Relif Organization kutoka Saudi Arabia, Majed Rashed , wakielekea kwenye hafla ya ufugaji wa kampeni ya upasuaji wa mtoto wa jicho iliyodumu wiki mbili kuanzia Septemba 25, mwaka huu mkoani Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, akitoa hotuba ya kufunga kampeni ya upasuaji mtoto wa jicho.
Mwakilishi wa Ubalozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania , Majed Al- Bagam , akisoma hotuba ya Balozi wake wakati wa hafla ya kuhitimisha kampeni ya upasuaji mtoto wa jicho.
Baadhi ya madaktari na watumishi wengine wakimsikiliza mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( hayupo pichani).
Baadhi ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho wakati wa kampeni ya wiki mbili kuanzia Septemba 25, mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kaunda suti nyeusi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni kutoka nje na ndani ya nchi.
Na John Nditi, Morogoro
Mkuu
wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, Oktoba 7, mwaka huu alikuwa mgeni
rasmi katika hafla ya ufungaji wa kampeni ya upasuaji wa mtoto wa jicho ,
pamoja na kuwapatia huduma wagonjwa wanaishi na upofu utokanao na mtoto
wa jicho.
Kampeni
hiyo pia ililenga kutoa tiba kwa magonjwa mengine ya macho , na
kuhamasisha wananchi kufuatilia huduma za macho bila kusubiri kampeni
hizo , ambapo kampeni hiyo ilihusisha Wilaya ya Kilosa, Kilombero ,
Morogoro ( Manispaa) na Ulanga.
Hata
hivyo katika kufanikisha kampeni huyo jumla ya madaktari watano kutoka
Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Kilosa na Hospitali ya Mkoa wa Iringa
waliweza kuwafanyia uchunguzi na jumla ya wananchi 12,080 walipatiwa
matibabu mbalimbali.
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro , Dk Godfrey Mtei, amesema mkoa imefanikiwa
kupata wafadhili mbalimbali wanaochangia kwa kiasi kikubwa huduma hizo za macho .
Aliwataka
baadhi ya wafadhili hao ni pamoja na International Islamic Relif
Organization kutoka nchini Saudi Arabia , Humanitarian Relief Foundation
kutoka nchini Uturiki, Bilal Muslim Mission, Lions Club ya Sweden,
Sightsavers, Halmashauri za Wilaya na Serikali kuu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni