Jumapili, 13 Oktoba 2013

WAZIRI MUKANGARA ATEMBELEA MAONYESHO YA WIKI YA VIJANA IRINGA

Waziri - 1Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (mwenye mavazi meusi) akiwasili katika viwanja vya maonyesho ya Wiki ya Vijana Shule ya Msingi Mlandege, Iringa akiwa ameambatana na viongozi wengine wa Wizara hiyo Katibu Mkuu Bi. Sihaba Nkinga (wa tatu kutoka kulia), Naibu Katibu Mkuu Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto),Mkurugenzi wa Utamaduni Prof. Herman Mwansoko (kulia) na Mkurugenzi wa Vijana James Kajugusi (wa pili kulia).
Waziri - 2Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (kushoto) akitembelea banda la Maonyesho ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere leo mjini Iringa.Waziri - 3Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (koti jeusi) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Sihaba Nkinga wakitembelea banda la maonyesho la wajasiriamali kutoka wilayani Bagamoyo wanaoshiriki maonesho ya Wiki ya Vijana mkoani Iringa.Waziri 5Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa leo mara baada ya kuangalia maandalizi ya sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge katika Uwanja wa Samora mkoani Iringa.
Waziri-4Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi.Sihaba Nkinga(kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kutengeneza bidhaa mbalimbali za asili zikiwemo sabuni za kuogea ya MKIPI yenye Makao yake Pemba na Zanzibar Bw. Mohamed Foum wakati alipotembelea banda la maonyesho la kampuni hiyo leo.
Picha na Aron Msigwa- MAELEZO.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...