Jumanne, 15 Oktoba 2013

ZOEZI LA KUONDOA MIFUGO WILAYA YA MOROGORO VIJIJINI LAZINDULIWA


Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera Kulia,akiwa na Mbunge wa Jimbo la Morogor kusini Mh Innocent Kalogeris wakati wa uzinduzi wa Zoezi la kuondoa Mifugo katika Wilaya ya Morogoro Vijijini.Lililozinduliwa Katika Kijiji cha Dutumi morogoro vijijini.Zoezi hilo limewashirikisha wadau mbalimbali.Baadhi ya wadau watakaoshiriki katika zoezi hilo ni Halmashauri ya wilaya ya Morogoro vijijini,Pori la udizungwa,Tanapa,Wami mbiki pamoja na Poro la selou.
 Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mh Said Amanzi akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Morogoro vijijini Mh Kibena Kingo
 
 Askari wa Kikosi cha wanyamapori wakiwa tayari kwa zoezi hilo mara baada ya Uzinduzi huo kufanyika 
Askari wea Jeshi la polisi watakaosimamia zoezi hilo tayari kwa kuanza zoezi la kuondoa mifugo  katika wilaya ya Morogoro Vijijini.
 Viongozi watakaosimamia na kuendesha zoezi la kuhamisha mifugo katika wilaya ya morogoro vijijini.
 Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Morogoro wakiwa kwenye uzinduzi wa zoezi hilo

 Wananchi wa kijiji cha dutumi Morogoro Vijijini wakiwa watulivu Kumsikiliza Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera wakati wa uzinduzi wa Zoezi hilo
Wananchi wa morogoro vijijini waliojitokeza kwa wingi wakati wa uzinduzi wa zoezi la kuondoa wafugaji waliovamia wilaya hiyo pamoja na mapori ya akiba.


Diwani akisikiliza kwa makini hotuba ya Mkuu wa mkoa wakati wa uzinduzi huo..

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...