Jumatano, 20 Novemba 2013

ABDULRAHMAN KINANA ATEMBELEA WILAYA YA SONGEA VIJIJINI

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi na wananchi wa Peramiho wakishiriki kubeba matofali ya ujenzi wa Zahanati ya Kahegwa wakati katibu huyo alipofanya ziara yake katika wilaya ya Songea vijijini jana kwenye jimbo la Peramiho linaloongozwa na Mh Jenista Mhagama ambapo amekagua miradi mbalimbali kwenye kata mbalimbali zikiweme zahanati vikundi vya ujasiriamali ikiwa ni pmoja na  kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM na kuhamasisha uhai wa chama, jimboni humo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Kahegwa baada ya kushiriki shughuli za kubeba matofali kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya Kahegwa,Katibu Mkuu aliwaeleza wananchi hao kuimarisha moyo wa kujitegemea  kwani maendeleo ya Tanzania yataletwa na Watanzania wenyewe na si wahisani.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akizungumza na mmoja wa wananchi aliyefarijika sana kwa kumsikia Katibu Mkuu akizungumza maneno ya msingi na yenye kutia moyo sana hasa katika suala la kujitegemea.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti kwenye zahanati ya Lusonga ambayo kwa asilimia kubwa imejengwa kwa nguvu za wananchi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,akiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Ndugu Jenista Muhagama ,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho na wakikata utepe wa kufungua jengo la Zahanati ya   Lusonga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisiliza taarifa ya kikundi cha akina mama wajasiriamali  watengeneza sabuni ambayo ilisomwa na Fransisca Andrea.
Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi la jengo la  Ofisi ya tawi la Mlandizi, Peramiho wilaya ya  Songea vijijini.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Peramiho ,wilaya ya Songea Vijijini  mkoani Ruvuma.
Mbunge wa Jimbo la Peramiho  Ndugu Jestina Muhagama akihtubia wakazi wa Peramiho na kuzungumzia matatizo sugu yanayo wasunbua wananchi wa jimbo lake hasa ukosekanaji wa Pembejeo na kutolipwa pesa wanayodai serikali kwa wakati.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Peramiho katika kata ya Masangu ambapo aliwapongea kwa kuwa wakulima wazuri

 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Tarafa Ndugu Salima Mapunda baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara.

 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya kufungua jengo la CCM Tawi la Masangu.
Katibu Mkuu wa CCm Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na masista  kutoka kanisa katoliki la Chikole,jimbo la Peramiho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...