MBUNGE wa jimbo la Morogoro mjini Aziz Abood amewataka
wanawake kuhakikisha wanabuni miradi iliokuwa na soko sambamba na kupata mafunzo kabla ya
kutekeleza miradi hiyo ili iweze kuwa na tija.
Abood alisema hayo jana wakati alipokuwa akifungua baraza la
jumuiya ya wanawake wa chama cha Mapinduzi CCm mkoa wa Morogoro.
Alisema kuwa ni vema kabla wanawake hao hawajaanzisha miradi
yao wawe wamepata mfunzo ya ujasiliamali ili kuweza kuendesha kwa ufanisi bila
kuingia hasara.
‘’ Wanawake wanaposhirikishwa katika masuala ya ujasiliamali
ni muhimu kupatiwa elimu kwanza, hii itasaidia kuweza kuendesha miradi yao kwa
faida’’ Alisema
Aidha Abood aliwataka wanawake hao kujiunga katika vikundi
mbalimbali ili kuweza kujihusisha na masuala ya kilimo na ufugaji miradi ambayo
ni rahisi kutekelezeka na kwamba ina soko la uhakika.
Kwa upande mwingine mbunge huyo aliwataka UWT mkoa wa
Morogoro kuhakikisha wanafika kwa wanachama wao kuanzia ngazi za chini ili kusikiliza kero za wanachama wake badala ya kukaa ofisini na kuongeza kuwa chama
kisichotoka na kuangalia kero za wanacama wake ni chama cha viongozi.
Pia aliwahimiza kuhakikisha wanaongeza wanachama wengi zaidi
katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ili chama hicho kiweze kuendelea
kushika dola kwa uhakika zaidi.
Vile vile aliwataka madiwani kuhakikisha wanagomea miradi ya
maendeleo katika kata zao ambayo iko chini ya viwangi .
Naye katibu wa UWT mkoa wa Morogoro Tuhuma Lihepa Alisema
kuwa wameanda mkakati wa kuwa na miradi ya kilimo na ufugaji nyuki ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuondoakana
na dhana ya kuombauomba katika kuendesha
shughuli za jumuiya hiyo.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Morogoro Mariam Kiamani alisema
kuwa jumuiya hiyo mkoani hapa iko imara
na kwamba kamwe hawatayumbishwa na wapinzani.
Alisema kuwa UWT imejiimarisha katika ngazi zote na kwamba
kamwe hawawezi kuyumbishwa na vyama ambavyo havina sera wa dira na kwamba
anachofanya kwa sasa ni kuhakikisha jumuiya hiyo wanavunja makundi yote ya
uchaguzi ili kuweza kujiimarisha zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni