HUYU NI BREGEDIA NYAKARUNGU GRAYSON MKUU WA KIKOSI CHA KUSAKA DEMOKRASIA CHADEMA, LEO ALIFANYA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI MJINI MOROGORO KATIKA MGAHAWA WA PEOPLES ULIOPO ENEO LA SABASABA, ALITOA SIKU TANO HADI DESEMBA 1 MWAKA HUU KUWATAKA VIONGOZI WALIOONDOLEWA MADARAKANI KUREJEA KATIKA NAFASI ZAO NA ENDAPO WATAPUUZA WATAANZA MIKUTANO YA HADHARA KUWASIMIKA VIONGOZI WAPYA NA KILA KONA YA WATANZANIA WATAJUA.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
TANGAZO RASMI LA UASI,
Katika tangazo hili yamezingatiwa mambo matano.
(1) Dhana ya ukabila ndani ya Chadema.
(2) Kuhusu kutonywa.
(3) Hekaya feki ya kimangimeza.
(4) Dhana ya ugaidi ndani ya chama.
(5) Msimamo wa wapigania Demokrasia wanaoitwa dhidi ya wahafidhina na watiifu wao.
Ndugu wanahabari, leoni ni siku ya historia ya siasa za vyama vya upinzani Tanzania , siasa za upinzani Tanzania zimekuwa zenye kuendeshwa na kuamriwa na wanaodhani wanamamlaka kuliko mifumo ya uanzishwaji wake.
Nasema siki hii mpya kwa sababu mkakati tulionao , tunaenda kutekeleza ili kuziondoa kwenye mwenendo wa uendeshwaji wa kimila na usanii.
Mimi nina historia ndefu ndani ya Chadema kabla ya Mzee Slaa kujulikana, Kabla Zitto Hajawa mbunge na kabla ya Helkopta kuonekana kwenye anga za siasa za Tanzania na kabla Chadema haijawa maarufu.
Katika kila chama cha siasa kuna mfumo wa uendeshaji na taratibu zake kama ilivyo ndani ya Chadema , na kila taasisi inakuwa ba katiba pamoja na kanuni zake za kuendeshea mambo yake.
Hata Chadema tunayo katiba na kanuni hizo tena zimeainishwa kitaalam na kiuweledi sana.
Lakini ndugu zangu unaweza kuwa na kanuni na katiba ya aina fulani nzuri lakini ukakosa msimamiaji mzuri mwenye utashi chanya wenye nia chanya, matokeo yake utapata mivurugano isiyo na tija wala afya kwa taasisi.
Tukirejea kwa Mwalimu Nyerere aliongoza nchi kwa katiba hii tulionayo ingawa imekuwa ikifanyiwa marekebisho lakini tunapata historia ya uongozi mzuri wake, katika katiba ambayo leo tunasema kuwa ndiyo inawapa mwanya viongozi wetu kuiba na kufanya ufisadi huku tukisahau suala la utashi.
Chadema kinajitumbukiza kwa umma kama chama chenye malengo na nia ya kutwaa dola wakati wowote kikitumia mbinu za aina mbalimbali kwenye jamii kikionyesha kina machungu na wala rushwa, mafisadi,walanguzi, kikihubiri Demokrasia majukwaani na kinalilia uwazi na serikali katika uendeshwaji wa mambo yahusuyo nchi.
Lakini kinachosikitisha kuona Chadema kinashindwa kuonyesha mfano ndani yake chenyewe,
kila anayethubutu kuhoji juu ya matumizi ya rasilimali za chama au pesa za chama au mgawanyo wa rasilimali mtu huyo huitwa msaliti au ametumwa na CCM.
Viongozi wetu wa Chadema wanahoji serikali na matumizi ya pesa wakataka uwazi na usawa leo wanataka kutonywa mapema ili wafanye marekebisho ya kuficha uovu wa matumizi ya fedha?
Zitto kama kiongozi anayejipambanua asingeweza kuwatonya ili wafiche uchafu huu huku akitengeneza nafasi ya kuumiza vyama vingine , hii ni dalili udikteta.
Na kwa sababu aligusa mkia wa mfalme wa NGE lazima ang'atwe.
Tunapaswa kujiuliza ni kwanini Zitto alishambuliwa sana na viongozi wa chama baada ya yeye kutoa msimamo na mazimio ya kamati ya PAC?
Hayo ni baadhi ya nukuu za maneno yaliopo katika waraka wa Brigedia huyo anayejiita wa waasi.
kikubwa alichozungumzia ni jinsi gani mwenyekiti wa chama hicho Mbowe anavyojilimbikizia madaraka hata ya ununuzi wa vifaa ambao ungeweza kufanywa na watu wengine wenye taalamu hiyo.
Alisema kuwa awali katika uchaguzi mkuu Mbowe alipotaka itumike helkopta katika kampeni hizo walidhani ni kiongozi bora ambaye anakipenda chama chake na kwamba anajitolea lakni cha kushangaza ni pale baada ya uchaguzi kuwaletea bili ya shilingi milioni 500 kutaka alipwe kama gharama ya uendeshwaji wa helkopta hiyo.
Lakini kingine anachozungumzia kiongozi wa waasi katika chama hicho ni kwamba wanachama wengi sasa wamechoshwa na uongozi wa Mbowe na kwamba kilichotakiwa ni kuondolewa jambo lililomfanya kuongia woga kana kwamba zitto angeweza kuchukua nafasi hiyo na hivyo kuamua kumdhibiti kabla ili badae aonekane hana sifa kutokana na kashfa hizo mbinu ambazo tayari wamezibaini.
Hata hivyo aliwataka watanzania kutoadharau mbinu za ugaidi na kwamba wanapopata taarifa wasidharau kwani Chadema wamekuwa na mbinu chafu za uharifu na kwamba wanaweza kufanya matukio mabaya ya uharifu na kusingizia CCM ndio wamefanya hivyo.
Amesema yeye ametumiwa ujumbe wa kumtishia maisha baada ya kutoa waraka huu hivi karibuni na tayari ameshatoa taarifa polisi ili dola iweze kujua na kuwafutilia watu wenye kutoa vitisho hivyo ndani walioko ndani ya Chadema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni