Jumapili, 22 Desemba 2013

WAKULIMA WATAKIWA KUTUMIA MBOLEA MINJINGU MAZAO.

unnamed_1_fe8fa.jpg
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr Christin Ishengoma akiongea na waandishi wa Habari katika ofisi ya mkoa

unnamed_2_6dbcd.jpg
Akitoa ujumbe wa heri ya kriss masi na mwaka mpya pamoja na mikakati ya utekelezaji nakaulimbiu ya (Mabadiliko kwa Hraka)
Na Mnyalu,
Iringa,Mkuu wa mkoa wa Iringa,Christine Ishengoma amewataka wananchi mkoani hapa kutumia mbegu bora,Mbolea ya kupandia na kukuzia hasa kilimo cha mahindi na mpunga ili kupata mazao bora.Ishenoma alitoa wito juo wakati alipokutana na waandishi ofisini kwake na kusema kuwa tayari pembejeoi zipo katika Halmashauri zote,ni vizuri wananchi/wakulima watumie vitu mbegu bora na mbolea ili kujikwamua katika janga la njaa.
Alisema kuwa wakulima watambue kua kipindi hiki cha mvua wapande mazao mapema ili kujihakikishia uhakika wa chakula.
"Katika maeneo ya uzoefu wa kupata mvua chache,pandeni mazao yanayovumilia ukame kwa kasi,mazao tunayohimiza kupanda yanayovumilia ukame ni mtama,muhugo,viazi vitamu na ulezi"alisema Ishengoma
Hata hivyo aliwasisitiza wananchi kuwa kila familia ipande zaidi ya ekari 2 ya zao moja au jingine ili kupata chakula cha kutosha na kuepuka adha ya kuomba chakula.
Pia aliwaagiza mawakala wote waliochguliwa kufikisha pembejeo za kilimo vijijini kwa wakulima,ili kila mmja anufaike na fursa hii.
Mwisho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...