Jumatatu, 27 Januari 2014

KIKWETE AAGIZA MADC MVOMERO, KILOSA NA GAIRO KUMPATIA TAARIFA SAHIHI ZA WAHANGA WA MAFURIKO KWA MAJINA



 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili katika eneo la Dumila wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro kwaajili ya kuwatembelea wahanga wa mafuriko na kujionea hali halisi.
 Rais Kikwete akitembela maeneo mbalimbali yaliokubwa na mafuriko hayo.
 Rais  Kikwete akiwa katika daraja la Mto mkundi lilopo Dumila Kilosa ambalo lilikatika kutokana na mafuriko.
 Nilazima tuangalie jinsi gani ya kufanya ili kuzuia mafuriko haya yasiwe na athari kubwa kama hizi. Kikwete akitoa malekezo kwa viongozi wa mkoa na wilaya za Gairo, Kilosa na Mvomero ambazo zimekubwa na mafuriko hayo.
 Mheshimiwa mimi ni muasisi wa chama miaka dahali sasa, nimekubwa na mafuriko kila kitu changu kimesombwa hadi kadi yangu ya chama, Salma Matewele akimwambia Kikwete.
 jamani poleni sana na mafuriko yaliowakubwa, kikwete akiwaambia wahanga wa mafuriko hayo katika eneo la Magole ambako ndiko walipoweka katika kambi.
 Mheshimiwa hapa tuna kontena tatu za dawa, hakunatatizo kabisa, mganga mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Mtei akimwambia kikwete.
 Wananchi waliofurika katika eneo la Mateteni kwaajili ya kumsikiliza kikwete kufutia mafuriko hayo.
katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Rojas Romuli akiwa na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilosa nasoro Udelele 
RAIS Jakaya Kikwete amewabana  wakurugenzi wa halmahsuri na wakuu wa wilaya za Kilosa, Mvomero na Gairo kuandaa taarifa sahihi ya wananchi walioathirika na mafuriko kwa idadi sahihi sambamba na majina ya wananchi hao  na kutaka apatiwe taarifa hiyo kesho mapema.


Rais Kikwete alisema hayo Janauri 27 mwaka huu wakati alipotembela katika eneo la Magole wilayani  Kilosa kuwapa pole wahanga hao na kujionea hali halisi ya mafuriko hayo.


Kikwete alisema kuwa kutokuwa na takwimu sahihi  na majina ya watu hao kutasababisha misaada hiyo kuwafikia  watu ambao hawajaathirika na hivyo kushindwa kuwafikia wahanga halisi.


‘’  Ni lazima mjiridhishe  kwa kuwatambua watu kwa majina na jinsia zao, hivi nikisema sasa hivi mkanionyeshe hao watu wapo’’ Alihoji Rais.


Alisema amelazimika kusema hayo baada ya mkuu wa mkoa wa Morogoro  Joel Bendara kusoma taarifa ya maafa hayo kuwa hadi sasa wananchi wapatao 12472 hawana makazi ya kuishi kutokana na mafuriko  huku akidai kuwa , idadi ya kaya zilizoathirika 2759,nyumba zilizozungukwa na maji 2922 na nyumba zilizobomoka ni  1141.


Alisema kuwa kutokuwa  na majina hayo kunamtia mashaka yeye kuwa takwimu hizo huenda sio sahihi jambo lililomfanya kuwataka kuhakiki upya na kutoa taarifa hiyo ifikapo Kesho.


‘’Uongozi unapimwa wakati wa matatizo, kutokuwa na majina na idadi sahihi kunaonyesha jinsi  gani msivyowajibika katika kutekeleza majukumu yenu’’ alisema.


Alisema kuwa  wakati wa mafuriko kama hayo yaliotokea mwaka 2009 wilayani Kilosa Mkuu wa wilaya wa wakati huo Halima Dendegu aliweza kufanya vizuri  kwa kuwa na idadi sahihi na kamili.


‘’ Halima alifanya vizuri wakati ule  japo alikuwa mwanamke, nyie hapa wanaume mnashindwa , wakati ule Halima alisimamia vizuri mkaanza maneno yenu ya hovyo, mlimsema kwakuwa alikuwa mkali,, Alisema


Hata hivyo Kikwete aliwataka wenye viwanda vya magodoro hapa nchini wanawapatia magodoro hayo ili yaweze kutumika kwa wahanga hao na kwamba hata kama hakuna fedha watalipwa badae.


Alisema kuwa chakula kipo cha kutosha na kwamba hakuna mwananchi ambaye atakufa kwa njaa na lengo la serikali ni kuhakikisha kila mwananchi anapata hudmua muhimu kama chakula, malazi na dawa pamoja na maji safi.


Alisema kuwa serikali itahakikisha huduma hizo zote zinapatikana kwa kipindi chote hiki  ili kuokoa maisha ya wananchi hao.


Alisema kuwa alipokea taarifa kutoka kwa mganga mku wa mkoa wa Morogoro kuwa hadi sasa wametibiwa wananchi 300 na kwamba magonjwa yanayosumbua ni kichomi na nimonia ambayo yanasabishwa na kulala chini jambo ambalo tayari ameagiza kila mwananchi kupatiwa gororo ili kuepuka magonjwa hayo.


Pia aliagiza uongozi wa wakala wa barabara mkoa wa Morogoro kuhakikisha wanatoa magogo na miti ilioziba katika mito na mifereji ili kuepuka maafa kama hayo katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendela kunyesha.


Alisema kuwa mafuriko kama hayo sio mara ya kwanza kutokea kwa wilaya ya kilosa hivyo ni lazima wananchi na serikali kwa ujumla ikachukua tahadhari  ili kuepuka maafa kama hayo kutokea.

Kwa upande mwingine Rais huyo alisema kuwa atayatumia majeshi ya hapa nchini katika ujenzi wa nyumba za muda badala ya kuzitumia halmashauri ambazo zimekuwa na milolongo mingi  ambayo itatoa mianya ya wizi wa vifaa hivyo vya waathirika.


‘’ Ukizitumia halmashauri  waanze kutangaza zabuni, hapo bado watu hawajafikiria  kila mtu atapata nini, hakuna kitakachofanyika, wanajeshi hao tuliwatumia  hata katika mafuriko ya 2009 yaliotokea Kilosa na walifanya vizuri na sasa tutawatumia tena alisema.


Awali mkuu wa mkoa wa Morogoro alisema kuwa tayari walishanza kupokea misaada mbalimbali ikiwamo ya  milioni 50,000 kutoka ofisi ya waziri mkuu, milioni 10,000 kutoka Islamic Foundationi sambamba na dawa  za milioni 80,000 kwaajili ya magonjwa mbalimbali.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...