Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Inocent Karogeries akiongea kwenye
warsha ya siku moja ya wadau kujadili taarifa ya tathimini ya athari
za kijamii na mazingira ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Ngerengere
hadi Kidunda pamoja na mtambo mdogo wa kuzalisha umeme na njia ya umeme
kutoka Kidunda wilaya ya Morogoro hadi Chalinze , warsha hiyo
imefanyika katika hotel ya kitalii ya Nashera mjini hapa.
Muu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Mecksadik akiongea juu ya mafanikio
ya mradi huo wa maji katika miko ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro,
ambapo amesema wananchi wa Dar wanatumia zaidi ya lita peke yake
wanatumia lita milioni 450 kwa siku.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza akiongea wakati wa warsha hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akifungua warsha hiyo ambapo
alisisitiza jinsi ya utunzaji wa mazingira ili kuhakikisha maji
yanapatikana kwa wingi katika mikoa hiyo ili kuepuka kutumia maji ya
visima ambapo mengine hutumia gharama kubwa kuyatibu.
Katibu mkuu wizara ya maji mwandisi Bashir Mrindoko akiongea wakati wa warsha hiyo.
Mwenyekiti wa badi ya DAWASCO Eva Sinale akiongea wakati wa warsha hiyo
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakifutilia kwa makini ufunguzi wa warsha hiyo.
Wajumbe wa mkutano huo wakiwa makini kufutilia warsha hiyo.
Mbunge wa jimbo la Morogoro kusini Inocent Kalogeries ameitaka Serikali
kuharakisha malipo ya fidia ya wananchi wa eneo linapotarajia kujengwa
bwawa la maji la Vidunda ili kuondokana na kero hiyo.
Alisema hayo wakati wa warsha ya kujadili taarifa ya tathimini ya
athari za kijamii na mazingira ya mradi wa ujenzi wa barabara ya
Ngerengere hadi Kidunda na mtambo wa kuzalisha umeme na njia ya umemem
kutoka kidunda hadi Chalinze .
Alisema kuwa mpaka sasa kuna kero hiyo kwa wananchi wake na kwamba
wanakosa majibu wao kama wanasisas juu ya fidia za wananchi hao.
Hata hivyo alisema kuwa kutokana na umuhimu wa bwawa hilo atahakikisha
anawashawishi wabunge wa mikoa ya Dar, Pwani na Morogoro kuhakikisha
wanapigania bajeti ya maji kuongezwa ili kusaidia ujenzi huo na fidia
za wananchi hao kwa haraka.
Katibu mkuu Muhandisi Bashiri Mrindoko alisema kuwa fidia kwa wananchi
hao ni bilioni 3.6 ambapo alidai kuwa ujenzi wa bwawa na barabara hiyo
kwa kiwango cha changarawe pamoja na umeme huo utagharimu kiasi cha dola
za Marekani milioni 160.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni