Jumatano, 16 Aprili 2014

BODABODA WAJIAJIRI WENYEWE KWA KUNUNULIANA PIKIPIKI 8 MORO

Vijana wa Bodaboda wakiwa katika picha ya pamoja na diwaniwa  wa kata ya Kingo Fidelis  Tailo baada ya kukabidhiwa pikipiki 8 walizonunuliana kutokana na michango yao.
Habari zaidi soma hapa
DIWANI wa kata ya Kingo katika manispaa ya Morogoro Fidelis  Tairo amewataka vijana wa Bodaboda kuepuka kufanya matukio ya uharifu na badala yake wawe walizni wa watu wanaofanya uharifu.
Alisema hayo  jana wakati akikabidhi pikipiki 8 za kikundi cha Nunge bodaboda zenye thamani ya shilingi milioni 13.2 zilizonunuliwa na vijana hao kutokana na michango yao.
Alisema kumekuwa na dhana  kuwa bodaboda wengi ni waporaji na waharifu na kwamba dhana hiyo ni vema wakaifuta ili kujenga uaminifu kwa wateja wao.
‘’ Mimi kama diwani wa kata hii nisingependa kukuta kijana wangu amejitumbukiza katika matukio ya kiarifu, fanyeni kazi za uhalali’’ Alisema.
Alisema serikali ya  chama cha Mapinduzi inatambua umuhimu wa biashara ya usafiri wa bodaboda na ndio maana imewaondolea kodi kwa lengo  la kuwafanya vijana wengi kuweza kujiajiri na kuepuka tabia ya kukaa vijiweni bila kazi hali inayosababisha kuingia katika makundi yasiofaa.
Kwa upande wake katibu wa kikundi hicho Dickson Paskari alisema mafanikio hayo waliyapata baada ya kukaa na kubuni kitu cha kufanya ili kuweza kujiajiri wenyewe na kupata kipato kinachotesheleza.
‘’ Tulianza kwa kuchanga kiasi cha shilingi 6000 kila siku kwa watu 8 na kila  mwezi tuakawa tunanunua pikipiki moja tunampatia mmoja anaanza kazi’’ Alisema
Alisema awali  walipoanza vijana wenzao waliwabeza kuona kuwa hawatafanikiwa na kwamba waliongeza juhudi ili kuhakikisha nia yao haiishii njiani.
Alisema kwa sasa wanampango wa kusajiri kikundi chao ili kuweza kufanya shughuli za kiuchumi zaidi na kwamba lengo ni kusaidiana katika kujikwamua kiuchumi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...