





PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA.
Na Benedict Liwenga – MAELEZO
SHIRIKA la Utangazaji Tanzania (TBC) na Shirika la Radio ya Kimataifa ya Jamhuri ya Watu wa China (CRI) leo kwa pamoja yameshirikiana katika sherehe ya Uzinduzi wa Tamthiliya ijulikanayo kwa jina la MAPENZI NA FURAHA YA KIJANA (Jin Tai Lang) ambayo imechezwa na China na kuwekwa sauti kwa lugha ya Kiswahili na wasanii wa Tanzania.
Sherehe hiyo imefanyika leo katika Viwanja vya TBC ikishuhudiwa na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Elisante Ole Gabriel akiwemo Mwakilishi wa Balozi toka Ubalozi wa China nchini Tanzania, Wajumbe wa Bodi ya Wakaurugenzi TBC, Mkurugenzi Mkuu Star Media Tanzania, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara mbalimbali na wafanyakazi.
Hatua ya uzinduzi wa sherehe hiyo ni matokeo ya utekelezaji wa Sera ya Serikali ya kujenga mahusiano na ushirikiano na nchi rafiki kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo habari, Utamaduni na michezo.
“Pamoja na kutekeleza sera za Serikali pia TBC tunatambua umuhimu wa kuwa na michezo ya kuigiza ambayo inazingatia utamaduni wa Watanzania na niwahakikishie kuwa Tamthiliya hizi zimeonesha hali hiyo.”. Alisema Mkurugenzi Shirika la Habari Tanzania Clement Mshana.
Mashirika ya habari ya TBC na CRI yamekuwa mstari wa mbele katika kuimarisha ushirkiano nah ii ni mara ya tatu kuwa na Tanmthiliya ya Kichina iliyowekwa sauti kwa lugha ya Kiswahili ambapo mwaka 2012 kulikuwa na tamthiliya ya MAU DOU DOU NA VISA VYA MAMA WAKWE ZAKE, ikifuatiwa na tamthiliya mbili nyingine ya MAISHA YA MAMA na FURAHA YA BABA ambazo zote zimepata umaarufu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni