Naibu katibu mkuu wa CCM Mwiguru Nchemba akipokelewa wilayani Gairo
alipokwenda jana kwa ziara yake ya siku moja wilayani humo.
Nchemba akisalimiana na wananchi wa wilaya ya Gairo.
Nchemba alipowasili katika ofisi ya CCM wilaya ya Gairo ambapo
alikutana na kamati ya siasa ya wilaya hiyo kabla ya mkutano wa hadhara.
Mkuu wa wilaya ya Gairo Khanifa karamagi akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ialani kwa Nchemba katika kikao cha kamati ya siasa.
Nchemba wakati akielekea katika mkutano wa hadhara
Nchemba akisalimiana na wananchi wa Gairo waliofurika katika mkutano huo
Mwiguru akizungumza na wananchi katika mkutano huo wa hadhara.
Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Rojas Romuli akizungumza kabla ya kumkaribisha mwiguru katika mkutano wa hadhara Gairo.
Awali Mwiguru alipowasili katika ofisi za CCM akivalishwa skafu.
habari zaidi soma hapa
NAIBU katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi CCM Mwiguru Nchemba
amesema wazee wanaofuta misingi ya kudumisha amani na utulivu wanchi alioacha
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wataheshimiwa na kuenziwa na chama hicho
na kwamba wale wanaokiuka wabezwe kwani hawana nia njema na nchi.
Mwiguru ambaye pia ni naibu waziri wa fedha alisema hayo jana wakati wa ziara yake wilayani
Gairo ambapo alifanya mkutano wa hadhara kuzungumzia kero kubwa ya maji
inayokabili wilaya hiyo.
‘’ Wazee wote ambao wanafuata misingi ya baba wa taifa
kudumisha amani na utulivu wan chi CCM itawaheshimu na kuwaenzi, lakini wale
ambao wakati baba wa Taifa alikuwepo wakawa wanajificha kwa unafiki wao na sasa
wameona kuwa hayupo wajitokeze na kutaka kuvuruga amanni na utulivu tulionao
hatuwawafumbia macho’’ Alisema
Alitolea mfano mmoja wa wazee hao ni Jaji Warioba ambaye
alipewa heshima ya kukusanya maoni ya katiba na kazi hiyo alishakamilisha
lakini cha kushangaza bado kila kukicha anakaziania kuwepo kwa Serikali tatu
jambo ambalo kamwe CCM halitakubali.
‘’ Huyo mzee ni waajabu kweli, alipewa kazi ya kusimamia
ukusanyaji wa maoni ya katiba lakini sasa kila kukicha unamwona kwenye vyombo
vya habari akililia serikali tatu, hana nia njema na serikali yetu , msimamo wa
CCM ni serikali mbili tuu’’ alisema
Aliwataka vijana kutambua kuwa serikali tatu ni mzigo ambao
haubebeki na kwamba watakaoumia ni watanzania kwa kuongezewa kodi mara dufu ya
hivi sasa.
‘’ Kwa sasa tunahangaika kutafuta ajira kwa vijana, hizo
fedha za kuendeshea serikali tatu badala ziende kwenye mambo ya maendeleo
na ili vijana waweze kupata ajira ‘’
alisema
Alisema kuwa kwa sasa
kwa sasa pato la taifa ni tririoni 7.7 na kati ya hizo tririoni 4
zinatumika kwa kulipa mishahara ya wafanyakazi
na zilizobakia ndio fedha za maendeleo.
‘’ Sasa hii serikali ya tatu ikija hizi fedha za maendeleo
ndio ziachuhudumia huko na kwamba fedha za maendeleo tutegemee kwa wafadhili
hiyo inaingia akilini kweli? Alihoji
Hata hivyo alisema watahakikisha inakuwepo sheria itakayosimamia fedha za mfuko wa vijana
ambazo zitakuwa zinatoka moja kwa moja
badala ya kupitia katika mifumo mingine ambapo mara nyingi imekuwa
ikikwamisha.
Alifafanua na kusema
upo utaratibu wa kila halmashauri kutoa fedha za mfuko wa vijana ambao
kwa asilimia kubwa hazifikii walengwa kama ilivyokusudia na kwamba sheria hiyo
itasaidia kubana mfumo huo na hivyo fedha kufikia vijana moja kwa moja.
Wakati huo huo alisema
NAIBU waziri wa Fedha Mwiguru Nchemba ametangaza vita dhidi
ya matajiri wanaokwepa kodi kwa kushirikiana na mawakala na watumishi wa Serikali na kwamba ameomba
kupewa taarifa ili aweze kupambana nao.
Mwiguru alisema hayo jana wakati wa ziara yake wilayani
Gairo mkoani Morogoro alipokwenda kusikiliza kero ya maji kwa wananchi wa
wilaya hiyo.
‘’ Tunaingia rasmi kwenye vita ya wakwepa kodi, kama kuna
mawakala, watumishi wanaoshirikiana na
matajiri hao tupeni taarifa ili tuwashughulikie, hatuwezi kuzoza kodi kwa wauza
vitumbua huku matajiri wanakwepa kodi’’ Alisema
Alisema wanaandaa sheria ya kufuta misamaha kwa ya kodi kwa
watu ambao hawastahili sambamba na kuweka sheria bitakayosimamia kuziba mianya
ya ukwepaji wa kodi.
‘’ Wapo matajiri ambao ikiwekwa kodi wanawatumia wananchi
kulalamikia ili wafutiwe kwa kigezo cha kutokuwa na uwezo, sio watanzania wote
hawana uwezo ambao labda ukiweza kodi kwenye simu washindwe kulipa, mbona milio
ya simu wanakwatwa fedha lakini hawalalamiki , hii tumeshaibaini na sasa
tutaishughulikia’’ Alisema
Hata hivyo alisema kuwa wanaangalia uwezekano wa kupekela sheria ya usimamizi
mzuri wa fedha za Serikali .
Kwa upande mwingine Mwiguru aliwatoa hofu wananchi wa Gairo
atahakikisha wanapatiwa visima vya maji vya muda wakati wakisubiri mradi
mkubwa unaofadhiliwa na benk ya dunia
ambao kwa sasa unasuasua kutokana na kuwepo na maji ya chumvi katika yvanzo
vilivyokusudiwa kwaajili ya mradi huo.
Alisema kwa sasa amepata taarifa kuna maji yanayotoka katika
mto uliopo jirani na mradi huo na kwa kuaznia watatumia kiasi cha shilingi
milioni 300 za fedha za ndani kupata visima hivyo huku juhudi za kuhakikisha
chujio la kuchuja maji ya chumvi zinaendela kufanyika.
Alisema tatizo la maji
ni ajenda tofauti na inatakiwa kushughulikiwa na kupewa uzito wa kipekee
na kwamba isihusishwe na masuala ya kisiasa kama ambavyo wapinzani wamekuwa wakitumia
mwanya huo kwa sasa.
Alisema serikali inatambua umuhimu wa maji kwa wananchi wake
na ndio maana hata katika bajeti ya mwaka huu fedha nyingi zimeelkezwa katika
miradi ya maji ili kuhkikisha wananchi wanaondokana na dhana hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni