Maria
Said mama mkubwa wa Nasra, katikati ni baba mzazi wa Nasra, Rashidi
Mvungi, na kulia ni mume wa Mariam Said wakiwa katika ofisi za ustwawi
wa jamii mjini Morogoro baada ya kukamatwa na kufikishwa polisi kwa
tuhuma za kumficha mtoto huyo ndani ya box kwa miaka 4 baada ya mama
wa mtoto huyo kufariki dunia kwa ugonjwa wa malaria .
Muuguzi
katika Wodi ya watoto hospitali ya rufaa ya Morogoro akimuhudumia mtoto
Nasra Said mara baada ya kufikishwa hopsitalini hapo kupatiwa matibabu.
Mtoto Nasra akiwa katika wodi ya watoto hospitali ya mkoa wa Morogoro anakopatiwa matibabu kwa sasa.
Habari zaidi soma hapo chini.
Mtoto Nasra akiwa katika wodi ya watoto hospitali ya mkoa wa Morogoro anakopatiwa matibabu kwa sasa.
Habari zaidi soma hapo chini.
MUME na mke wanashikiliwa na polisi mkoani hapa kwa tuhuma za kumficha mtoto
kwa miaka 4 ndani ya Box .
Kamanda
wa polisi mkoani Morogoro Leonard Paul alisema tukio hilo lilibainika Mei
20 mwaka huu majira ya saa 4.45 Asubuhi katika eneo la mtaa
Azimio kata ya Kiwanje Ndege Morogoro.
Alisema
majirani walizingira nyumba ya mwanamke ajulikanae kwa jina la Maria Said na
kutaka kuvunja ndipo polisi walipopata tarifa na kufika katika nyumba hiyo na
kukuta mtoto huyo akiwa katika box.
Alimtaja
mtoto huyo aliyejulikana kwa jina la Nasra Rashid Mvungi mine na nusu
ambapo polisi ilichukua jukumu la kupeleka kesi hiyo Ustawi wa jamii ili
kuendela nayo.
Afisa
Ustawi wa jamii katika ofisi ya mkoa wa Morogoro Oswing Ngungamtitu alisema
mtoto huyo alipelekwa hopsitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa sababu
alionekana kuwa na afya dhoofu.
Alisema
alilazwa na kwamba kwa sasa yupo chini ya uangalizi wa ustawi wa jamii huku
wakiwachukulia hatua za kisheria walezi wa mtoto huyo Mariam Said na Mume
wake Mtonga Omari.
Baba
mzazi wa mtoto huyo alisema yeye ana mke na watato wengine wa ndoa na
kwamba hakuwahi kumwambia mkewe kama ana mtoto wa nje hivyo ilikuwa vigumu kumchukua
mtoto huyo na ndipo alipomkabidhi mama mkubwa wa mtoto huyo.
Alisema
kila mara alikuwa akifika kumwona mtoto mama huyo alimwambia mtoto kalala na
hivyo kushindwa kumwona na kujua hali halisi hadi siku ya tukio na kwamba
alikuwa akimpatia matumizi ya mtoto huyo.
Ofisa
mtendaji wa kata hiyo Dia Zongo alisema akiwa katika kazi za kawaida
katika Mtaa wa Azimio, alipata taarifa kutoka kwa majirani kuwa mwanamke huyo,
alimficha mtoto Nasra ndani ya boksi na kwamba hamfanyii usafi wala kumtoa nje.
Zongo
alisema baada ya kupata taarifa hizo, alimtafuta Mwenyekiti wa mtaa huo, Tatu
Mgagala na kuongozana naye hadi kwenye nyumba hiyo na kuanza kumhoji
mwanamke huyo ambaye alikuwa akijibu kwa kubabaika na kushindwa kueleza ukweli
juu ya kuwepo kwa mtoto huyo.
Zongo alisema wakati mtuhumiwa akiendelea kujibu
maswali, ghafla mtoto huyo alipiga chafya na kuanza kukohoa hali iliyowapa
wasiwasi na kuamua kuingia chumbani kwa mwanamke huyo kwa nguvu na kumkuta
mtoto Nasrah akiwa ndani ya boksi nyuma ya mlango .
Ofisa
mtendaji huyo alisema wakati wakimtoa mtoto huyo kutoka ndani ya nyumba ya mama
yake huyo mkubwa, ghafla kundi kubwa la watu waliokuwa na fimbo na mawe,
walianza kumshambulia mwanamke huyo, kitendo kilichomlazimisha (mtendaji)
kutoa taarifa polisi.
Baada ya
kufikishwa katika kituo cha polisi mwanamke huyo alikiri kuanza kumlea
mtoto huyo tangu akiwa akiwa na umri wa miezi tisa na kwamba hatua hiyo ilikuja
baada ya mama yake, kufariki dunia mwaka 2010.
Mtuhumiwa
huyo alisema kwa mara ya mwisho, alimuogesha mtoto huyo Julai mwaka jana na
kwamba alikuwa akimwekea chakula na maji ndani ya boksi lililokuwa limewekwa
nyuma ya mlango wa chumba cha mwanamke huyo.
Hores Isaack Msaky Dk Mshauri wa watoto katika hospitali ya mkoa wa
Morogoro alikiri kumpokea mtoto huyo na kwamba tayari ameshaanzishiwa matibabu
ya awali .
‘’
Tulimfanyia vipimo vya awali mtoto amebainika kuwa na
Nimoni pamoja na utapia mlo na sasa ameshaanza matibabu’’ Alisema
Alisema
bado wanaendela na vipimo vingine vya XRay kubaini mtoto huyo alipata ulemavu
kwa kupigwa au alizaliwa hivyo.
Alisema
mtoto huyo anamaumivu makali sehemu ya mgongo na mikono na kwamba mwili wake
pia ni mteke kama wa mtoto mchanga hali inayowafanya kuendela kumfanyia
uchunguzi wa kina zaidi.
Baadi ya
mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa mama wa mtoto huyo alifariki dunia
miaka mine iliopita na kwamba Mariamu Ni mama mkubwa wa mtoto huyo.
Hata
hivyo majirani hao walidai wanahusisha tukio hilo na imani za kishirikina
kutokana na kwamba mama huyo anaakili timamu na analea watoto wake vema tofauti
na mtoto huyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni