Naibu meya wa manispaa ya Morogoro Lidya Mbiaji
akikabidhi dawati kwa mkuu wa shule ya msingi Bungo Roman Luoga huku
kaimu afisa elimu wa manispaa ya Morogoro Christopher Wangwe
akishuhudia.
Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro akiwa katika picha ya pamoja na
waratibu wa elimu kata, baada ya kukabidhi madawati ya Plastiki
yaliotokana na fidia ya fedha za Rada.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Mazimbu B wakifungua maboksi ya madawati hayo .
HALMASHAURI
ya Manispaa ya Morogoro imepokea
madawati 756 kutoka Serikali kuu yalionunuliwa kwa fedha za fidia ya Rada.
Madawati
hayo aligawiwa jana katika shule 9 za manispaa
hiyo sambamba na vitabu 127,867 vya masomo yanayofundishwa shule za
msingi.
Naibu Meya
wa Manispaa ya Morogoro Lidya Mbiaji alisema hayo jana wakati akikabidhi
madawati hayo kwa walimu wakuu wa shule hizo.
Aliwataka
wazazi na walezi wa watoto hao kuwajibika katika kuyatunza madawati hayo ili
yaweze kudumu na kuondokana na kero ya madawati.
Hata hivyo
aliwataka walimu wakuu wa shule zilizopatiwa madawati hayo kuhakikisha wanatoa
madawati hayo kwa wanafunzi ambao wenye kuweza kuyatunza .
Kaimu
mkurugenzi wa Manispaa hiyo Philemon Magesa alisema madawati hayo yamekuja
wakati manispaa hiyo ikiwa na upungufu wa madawati takribani 7000.
Alisema pamoja na kupata madawati hayo sio kigezo kwa wazazi na walezi kubweteka
katika zoezi la kuchangia suala zima la madawati.
Mwenyekiti
wa kamati ya huduma za jamii Zumo Makame alisema msaada huo utasaidia kuondoa
kero kwa wanafunzi ambao walikuwa wakikaa chini kwa kukosa madawati wakati wa
kusoma.
Alisema
kamati ya huduma za jamii inalenga kuboresha elimu na hivyo kuhakikisha
wanaondoa kero zote zinazokabili elimu ili kutoa fulsa kwa wanafunzi kufanya
vizuri katika masomo yao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni