Mkurugenzi wa fedha wa mamlaka
ya maji safi na taka Jiji la Dar es Salaam aliyesimama Didas Mwilawi,
Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Inocent Karogieris wapili kushoto
kwake, mkuu wa wilaya ya Morogoro Saidi Amanzi, Mwenyekiti wa
halmashauri ya Morogoro Kibena Kingo, na mkurugenzi wa halmashauri hiyo
Yona maki ,wakati wa kikao cha watendaji wa Dawasa na Halmashauri hiyo
kutoa maelekezo ya fedha bilioni 7.9 zitakavyoafikia wananchi
wanaofidiwa katika bwawa la Kidunda.
Baadhi ya wafanyakazi wa Dawasa wakifuatilia kikao hicho.
Wajumbe walioshirikia kikao hicho ambao ni wawakilishi wa wananchi wa Bwawa la Kidunda.
Mkurugenzi wa fedha wa Dawasa Mwilawi akitoa ufafanuzi juu ya mgawanyo wa fedha hizo.
Habari zaidi
Baadhi ya wafanyakazi wa Dawasa wakifuatilia kikao hicho.
Wajumbe walioshirikia kikao hicho ambao ni wawakilishi wa wananchi wa Bwawa la Kidunda.
Mkurugenzi wa fedha wa Dawasa Mwilawi akitoa ufafanuzi juu ya mgawanyo wa fedha hizo.
Habari zaidi
JUMLA ya sh
Bilioni 7.9 zinatarajiwa kulipwa na Mamlaka ya maji safi na Taka Jiji la Dar es Salaam (DAWASA) kwa wananchi wanaoishi karibu na
bwawa la Kidunda wilaya ya Morogoro.
Mkurugenzi wa fedha wa DAWASA Didas Mwilawi alisema hayo jana wakati
wa kikao cha watendaji wa Mamlaka hiyo na Halmashauri ya wilaya ya Morogoro.
Alisema
fedha hizo zitalipwa kwa utaratibu wa hundi
kwa wananchi wote ambao tayari
walishahakikiwa na kupewa fomu ya fidia
namba 69.
‘’ Fomu hii
ilitolewa na maafisa ardhi wakati wa uthamini wa fidia na inayo kumbukumbu namba, mfidiwa atatakiwa
kuonyesha fomu hiyo kama ushahidi’’ Alisema.
Hata hivyo
alisema kwa wananchi walioko jirani na bwawa hilo watatakiwa kuhama ndani ya
miezi 6 huku wale wale ambao barabara imepita maeneo yao watatakiwa kuondoka
ndani ya miezi mitatu kupisha ujezi huo.
‘’ Ni lazima
tuanze kutengeneza barabara inayoanzia Ngerengere hadi katika bwawa hilo alafu
ndipo tuanze ujenzi wa bwawa’’ Alisema.
Mbunge wa
jimbo la Morogoro Kusini Inocent
Karogerie aliwataka wananchi hao kuhakikisha fedha hizo wanazitumia kujenga
makazi bora na sio kuzitumia katika matumizi mengine.
Mwenyekiti
wa halimashauri ya wilaya ya Morogoro Kibena Kiongo aliwataka viongozi kutowalazimisha wananchi
hao na kuwachgulia Benk ya kujiunga kwaajili ya zoezi hilo na badala yake
wawaache wenyewe wafanye maamuzi.
Naye
mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Morogoro Yona Maki alisema tayari
viwanja 1000 ( elfu moja vimeshapimwa kwaajili ya makazi ya wananchi hao.
Alisema watu
2600 ndio wanatakiwa kufidiwa katika zoezi hilo kwa upande wa barabra
itakapopita na wale wanaishi jirani na bwawa hilo.
Bwawa la
Kidunda linajengwa kwaajili ya kuchukua maji kutoka katika mto Ruvu kwaajili
ya kusaidia kuwa na uhakika wa maji
katika kipindi chote cha mwaka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni