Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akifungua mkutano wa 98 wa watayarishaji wa vipindi shirika la utangazaji la Taifa TBC.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo.
MKUU wa mkoa
wa Morogoro Joel Bendera amewataka watumiaji wa mitandao ya kijamii ,
kuacha tabia ya kutumia mitandao hiyo kwaajili ya kukashfiana , kutoleana lugha chafu na
kudhalilishana na badala yake itumike kwaajili ya kutoa elimu na burudani.
Alisema hayo
jana wakati wa mkutano wa 98 wa
watayarishaji wa vipindi vya elimu kwa umma kupitia shirika la Utangazaji
Tanzania TBC.
Alisema
mitandao hiyo kwa sasa watumiji wamekuwa wakitumia kinyume na malengo, kutokana
na kukosa nafasi katika vipindi mbalimbali vya Tv na radio.
‘’ Mara
nyingi mashirika ya utangazaji yamekuwa yakitoa nafasi kwa wataalam na
viongozi huku waiwasahau wananchi jambo
linalosababisha kutumia mitandao ya kijamii kuweka habari zao’’ alisema
Hata hivyo
mkuu huyo aliwataka watoa habari kuacha tabia ya kukwepa kutoa habari kwa
waandishi wa habari pale zinapohitajika kwani kufanya hivyo kunasababisha
kuandikwa kwa habari zisizo sahihi.
‘’ waandishi
wa habari sio watu wa kuwakimbia, wanapohitaji habari wapatie ili waweze
kuchuja na kuandika kile kinachofaa’’ Alisema
Hata hivyo
aliwataka waandishi wa habari kuacha tabia ya kuandika habari kwa zenye chuki na kulenga kumdhalilisha mtu bila
sababu yeyote.
Kwa upande
wake Mkurugenzi mkuu wa TBC Clement mshana aliwataka wasemaji wa wizara kujenga
tabia ya kuita vyombo vyote vya habari pale wanapotaka kutoa taarifa ya
uelimisha umma au zinapofanyika kampeni mbalimbali.
Alisema
lengo la mafunzo hayo ni kuboresha weledi wa utayarishaji wa vipindi mbalimbali
katika shirika hilo.
Kwa upande
wake mkurugenzi wa mfuko wa Pensheni wa
PSPF Adam Mayingu alisema mfuko huo kwa sasa mfuko huo una wanachama tegemezi
wapatao 400,000.
Alisema
lengo la kudhamini mafunzo hayo ni kuwafanya watayarishaji hao kuwa na uelewa
juu ya mfuko huo wa PSPF .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni