Ijumaa, 29 Agosti 2014

WAZEE KUNUFAIKA NA BIMA YA AFYA SASA

 Rose Ongara meneja mfuko bima ya afya Morogoro akikabidhi mashuka  220 kituo cha afya cha  Gairo kwa Rais Jakaya Kikwete wakati alipotembelea kituo hicho juzi.
Wafanyakazi wa mfuko wa bima ya afya wakiwa katika picha ya pamoja na Rais Kikwete, na viongozi mbalimbalimbali akiwemo mbunge wa jimbo la  Gairo Ahmed Shabiby, mkuu wa  wilaya ya Gairo Khanifa Karamagi, mganga mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Mtei.
habari zaidi soma hapa chini,





 RAIS Jakaya Kikwete amesisitiza umuhimu wa mfuko wa bima ya afya kwa wananchi na kutaka wazee waingizwe kwenye mfumo huo ili kuepuka kunyanyasika.

Alisema hayo jana wakati wa majumuisho  ya ziara yake yaliofanyika wilayani Gairo mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi katika wilaya zote sita za mkoa wa Morogoro.

‘’ Nendeni mkajifunze kule Kilindi wenzenu walifanya ujuzi gani wa kuwaingiza wazee katika mfumo wa bima ya afya, kwa sasa  malalamiko kwa wazee kwa wilaya ile hakuna tena’’ Alisema.

Alisema kama wilaya zote ziatafanikiwa kufanya hivyo malalamiko ya wazee kudharauliwa wakati wakihitaji matibabu  tutakuwa tumeyamaliza kabisa.

‘’ wazee wenyewe sio wengi kama watu wanavyotafsiri, watu wote tupo milioni 48, tuliozaliwa kabla ya muungano ni milioni 4 tu ambao ndo wazee sasa ni wengi hao tushindwe kuwahudumia’’ Alisema.

Alisema mfuko huo unasaidia sana katika suala zima la matibabu kwa kuwapatia huduma watu tegemezi 4 kwa kiasi cha shilingi 10,000 jambo ambalo ni dogo ukilinganisha na matibabu bila mfumo huo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...