Jumapili, 21 Aprili 2013

ABDURAHMAN KINANA AMALIZA ZIARA YAKE MOROGORO VIJIJINI LEO

1Ndugu Abdurahman Kinana Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM akitembelea shamba darasa la wananchi wapatao 180 kutoka Wilaya ya Morogoro Vijijini wanaosimamiwa na kupewa mafunzo ya kilimo bora na ufugaji bora na  Shirika la Maendeleo la Korea  KOICA, wakati alipotembelea mradi huo katika ziara yake ya kichama ya mkoa wa Maorogoro, ambapo leo alifanya ziara katika Wilaya ya Morogoro vijijini na kufungua mashina na matawi ya chama hicho huku akipokea wanachama wapya waliojiunga na  waliotoka vyama vya upinzani, Kulia anayezungumza na Abdurahman Kinana ni Kim Sun Ho Meneja Mradi huo wa KOICA Korea, Wananchi hao wanamiliki zaidi ya hekari 150 kila mmoja ana magunia  8 ya mahindi waliyovuna mwaka jana  huku wakiwa na kiasi cha shilingi milioni 50,ooo,ooo benki.(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWEBLOG) 2 
Mratibu wa mradi huo Mbwambo Apendaimani akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana juu ya utaalamu unaotolewa na shirika hilo kwa wakulima hao na ufugaji wa kisasa, Katikati ni Kim Sun Ho Meneja
Mradi 3 
Hapa akipata maelezo huku akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali wa CCM taifa na mkoa wa Morogoro. 5 
Katibu mkuu wa CCM Abdurahman Kinana akifungua shina la wakereketwa la Tekemelo Kiroka Morogoro vijijini 6 
Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi wa CCM Nape Nnauye akifurahia zawadi ya majogoo mawili aliyopewa na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Lucy Nkya 9 
Hapa akifungua tawi la Msala 10 
Akitembelea mahali patakapojengwa soko katika Kata ya Makuyuni Matombo Morogoro 12 
Abdurahman Kinana aliyeshika mfagio akiangalia kazi za mikono za wananchi wa Makuyuni 13 
Katibu Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana akichanaganya mchanga na simenti wakati alipotembelea ujenzi wa kituo cha afya cha Makuyuni Morogoro vijijini Leo. 14 
Wananchi wa kata ya Kiroka wakimsikiliza Abdurahman Kinana hayupo pichani wakati akizungumza 16 
Wanachama wapya wa CCM wakionyesha kadi zao juu baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa CCM  Abdurahman Kinana. 19 
Katibu wa NEC Oganizesheni CCM Dk. Mohamedapo  Seif Khatib akiwahutubia wananchi wa Mvuha Matombo hawapo pichani , kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro na Mbunge wa morogoro Kusini  Innecent Kalogeres. 21 
Wananchi wa Kata ya Mvuha Matombo wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye wakati akiwahutubia. 22 
Wanachama wapya wa CCM wakionyesha kadi zao mara baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Abdurahman Kinana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...