Alhamisi, 25 Aprili 2013

MAMA SALMA KIKWETE KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 40 YA JHPIEGO

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,wama, Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Jhpiego nchini Tanzania, Bi Maryjane Lacoste kwenye hoteli ya Doubletree huko Masaki kulikofanyika sherehe ya kutimiza miaka 40 ya shirika hilo tarehe 23.4.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Dr. Maryrose Giattas, Cervical Cancer Prevention Program Adviser wa Shirika la Jhpiego kwenye maonyesho ya huduma mbalimbali zitolewazo na shirika hilo. Maonesho hayo yalifanyika katika hoteli ya Doubletree ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 40 ya shirika hilo.
Mama Salma Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Dr. Hokororo wa shirika la JHPiego juu ya kuhifadhi vifaa vinavyotumika katika suala zima la afya ya mama na mtoto.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa na baadhi ya viongozi waliohudhuria sherehe ya kutimiza miaka 40 ya shirika la Jhpiego huko Doubletree hotel Masaki. Kulia kwa Mama Salma ni Dr. Leslie Mancuso, Rais na Mtendaji Mkuu wa Jhpiego akifuatiwa na Bi Sharon Cromer, Mkurugenzi wa Shirika la USAID nchini Tanzania. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Seif Rashid akifuatiwa na Dr Allan Damiba, Jhpiego Senior Vice President na wa mwisho ni Mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa Sophia Mjema, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa kwenye sherehe za kutimiza miaka 40 ya shirika la Jhpiego wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Mama Salma Kikwete.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akihutubia kwenye sherehe za kutimiza miaka 40 ya shirika la JHPiego kwenye hoteli ya Doubletree huko Masaki jijini Dar es Salaam tarehe 23.4.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwashirikiana na viongozi wengine kukata keki ya kutimiza miaka 40 ya shirika la Jhpiego zilizofanyika katika hoteli ya Doubletree. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa USAID Bi. Sharon Cromer, Rais na Mtendaji Mkuu wa Jhpiego Dr. Leslie Mancuso, Mama Salma, Bi Maryjane Lacoste, Mkurugenzi wa Jhpiego nchini Tanzania, Dr. Seif Rashid, Naibu Waziri wa Afye na Ustawi wa Jamii na Dr. Allan Damiba, Jhpiego Senior Vice President.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akigongainisha glass yake na Rais na Mtendaji Mkuu wa Jhpiego Dr. Leslie Mancuso ikiwa ni kusherehekea kutimiza miaka 40 kwa shirika hilo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipongezana na Rais wa Jhpiego Dr. Leslie Mancuso mara baada ya kukata keti ya kutimiza mika 40 ya shirika hilo katika sherehe zilizofanyika huko Doubletree hotel tarehe 23.4.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaaga kwa kuwapungia mikono washiriki waliohudhuria sherehe za kutimiza miaka 40 ya shirika la Jhpiego. PICHA NA JOHN LUKUWI 

Read more: http://audifacejackson.blogspot.com/2013/04/mama-salma-kikwete-katika-sherehe-za.html#ixzz2RSgCCvQj

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...